Waziri
wa Fedha Dkt William Mgimwa akikata utepe wa uzinduzi wa maabara ya
kisasa iliyogharimu milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji vya
Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui wakati Waziri huyo alipotembelea
Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika
vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kushoto ni Mbunge wa Jimbo Tabora
Kaskazini Mamlo Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa
Mradi wa Vijiji vya Milenia wa Mbola Dkt Gerson Nyadzi.
Waziri
wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16
vinavyotekeleza mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani
Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji
vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia
. Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano
ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi
huo. Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi
na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha. PICHA na GCU – HAZINA
…………………………………………….
Na Mwandishi wetu -GCU-Hazina- Uyui- Tabora
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa
amewataka wakazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora waliopo katika wa
utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa
Mbola kuufanya mradi huo kuwa endelevu kwa kutunza vizuri miradi yote
iliyoibuliwa kwa ajili ya uboreshaji wa maisha ya wananchi wa eneo hilo .
Waziri huyo alitoa kauli hiyo jana
wilayani Uyui mkoani Tabora mara baada ya kuzindua maabara iliyochini
ya mradi huo ambayo imegharimiu shilingi milioni 49 hadi kukamilika.
Alisema kuwa ni vema wananchi hao
wakahakikisha miradi yote iliyotekelezwa chini ya mradi wa vijiji vya
milenia wa Mbola inatunza vizuri ili iwe darasa la kufundishi vijiji
vingine hapa nchini katika utekelezaji wa malengo 8 ya milenia.
Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa
itasikitisha kuona kuwa mara baada ya muda wa mradi kuisha wa 2006-2012
na wafadhili ambao ni Milenia Promise Tanzania kumaliza muada wao na
miradi inakufa na kusema kuwa hatua hiyo haitakuwa nzuri.
Aidha alitoa wito kwa wanavijiji
wengine ambao hawapo katika mradi huo kwenda katika Kijiji cha
Ilolanguru wilayani Uyui ili wajifunze jinsi ya utekelezaji wa malengo
ya Milenia kwa kutumia juhudi za wananchi. Awali akitoa taarifa kwa Waziri wa
fedha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha alisema kuwa
katika utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya
Milenia wa Mbola wameweza kuboresha maisha yao katika vijiji 16 katika
eneo hilo.
Alitaja manufaa waliyokwishapata
ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa kutumia matofali ya kuchoma
na bati na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na fedha.
Mogoha aliongeza kuwa pia mradi
huo umewawezesha kupunguza tatizo la vifo vya watoto waliopo chini ya
maika 5 na mamawajawazito ambapo awali vifo vilikuwa wastani wa watoto
watatu(3) hadi watano (5) na wanawake wajawazito 3 hadi 5 katika kipindi
cha miezi mitatu lakini hivi sasa vifo ni wastani huo katika kipindi
cha miezi sita na wakati mwingine hakuna.
Alisema kuwa hatua hii imefikiwa
mara baada ya kuwaelimisha wananchi juu ya kutumia vyandarua na kuua
mazalia ya mbu na hivyo kupunguza malaria katika eneo hilo.
vilevile Mwenyekiti huyo aliongeza
kuwa kiwango cha wanafunzi wanaoishia njia(drop out) kimepungua mara
baada ya mradi huu kuanza kwani mbinu mbalimbali zimesaidia watoto wengi
kumaliza darasa la saba . Mbinu hizo ni pamoja na kutoa chakula kwa wanafunzi na kuhamasisha michezo mashuleni jambo liliwavutia watoto wengi.
kuhusu suala la maji alisema
wanaendelea vizuri ambapo wastani wa asilimia 60 ya wakazi wa eneo hilo
wanapata maji safi na salama. Mradi wa vijiji vya Milenia wa
Mbola unatelelezwa katika vijiji vya Ilolanguru, Isenga, Ngokolo,
Ulimakafu, Mpenge, Isila, Mbola, Kasisi A, Mabama, Ideka, Mbiti,
Msiliembe, Iberi, Inonalwa, Usagari, Msima na Migungumalo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)