Askari
Polisi wakimrejesha mahakamani mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa
mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten na Mwenyekiti wa Klabu
ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, marehemu Daudi Mwangosi, askari
wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) (aliyevaa
kofia nyekundu baaada ya kutoroshwa kizimbani kabla ya mahakama
kumaliza shughuli zake, picha ya chini ikimuonesha wakati akirudishwa
ndani ya mahakama leo.Picha na Francis Godwin-iringa
---
SAKATA la
mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa
mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi
Mwangosi limezidi kuchukua sura mpya baada ya askari waliomfikisha
mtuhumiwa huyo wa mauaji askari wa FFU mwenye namba G2573
Pasificus Cleophace Simoni (23) kumtibua hakimu na kuageza mtuhumiwa huyo
kurudishwa tena kizimbani kwa kudharau mahakama hiyo.
Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 5.35 kwa askari
hao watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja kumshusha
kizimbani mtuhumiwa huyo wa
mauwaji na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na
wanahabari waliokuwepo hapo lilitokea
mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo.
Huku bado mahakama ikiwa inaendelea kwa hakimu
kutaja tarehe ya kesi hiyo namba ya
mauwaji kesi namba 1 ya mwaka 2012 mtuhumiwa wa mauwaji alishuka kizimbani huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula)na
miwani ya giza na kuanza kushuka
jukwaani kabla ya hakimu kumtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani
huku kabla ya mahakama kumalizika.
Wakati
hakimu huyo akijiandaa kusimama ili
kuhitimisha shughuli za kimahakama kwa siku
hiyo ghafla alijikuta anabaki na mwanasheria wa mahakama ,kalani wake ,wanahabari ,askari
mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa
huyo huku askari watatu wenye silaha na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha
mahakama hiyo.
“Mbona hao
askari wanamtoa mtuhumiwa bila utaratibu
wa mahakama hebu mwanasheria waambie
wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona wanafanya fujo mahakamani hao” alisikika akisemahakimu mkazi
wilaya ya Iringa Dyness Lyimo
Hata hivyo pamoja na jitihada za mwanasheria wa
serikali Adolf Maganda kuwaita
kwa sauti askari hao
kuwataka kumrudisha ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo bado askari
hao walizidi kukimbia na
mtuhumiwa kwenda nae mahabusu na baada ya dakika kama 5 hivi ndipo
mwanasheria huyo aliporejea na askari
hao na mtuhumiwa ambae hata hivyo
hakwenda kusimama kizimbani na
badala yake alikwenda upande wa kushoto wa mahakama hiyo ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya
mahakama kuanza na kuketi katika kiti huku akiwa amevaa miwani na kofia yake.
Kutoka
na tukio
hilo hakimu huyo alilazimika kuwahoji askari hao watatu kwa vurugu hizo
walizozifanya kwa kuwauliza swali moja
pekee kuwa wanaona walichofanya ni sahihi na askari hao kuomba msahama kuwa samahani mheshimiwa.
Mwendesha
mashtaka wa jamhuri Adolf Maganda aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe
nyingine na kutajwa tena kesi hiyo
ambayo ilitajwa Januari 27 na mtuhumiwa huyo kushindwa kufika kutokana na
tatizo la ugonjwa lililokuwa likimsumbua
.
Hata
hivyo mahakamani hiyo liahirisha kesi hiyo hadi Februari
14 mwaka huu kesi hiyo itakapofikishwa mahakani hapo kwa kutajwa tena.
Mtuhumiwa
huyo anatuhumiwa kumuua kwa bomu aliyekuwa
mwandishi wa habari wa Chanel Tena mkoa wa Iringa
marehemu Mwangosi septemba 2 Septemba mwaka jana katika kijiji cha
Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wakati wa vurugu kati
ya polisi na wafuasi wa Chadema .kinyume na kifungu cha sheria
namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai,
sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002
MWISHO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)