NAPE AUMALIZA UPINZANI RUNGWE MPYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NAPE AUMALIZA UPINZANI RUNGWE MPYA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ametembelea Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na Kuweka jiwe la Msingi la Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata hiyo pamoja na Kata ya Asante Nyerere.

Baada ya kuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutyoka katika kata za Asante Nyerere pamoja na Rugwe Mpya, wanachama ambao wamerejea CCM kutoka vyama vya upinzani hasa NCCR Mageuzi na Chadema.

Aidha Nape pia alipata fursa ya kuzungumza na Wajumbe wa Nyumba Kumi wa chama hicho, Wazee pamoja na Vijana waendesha Bodaboda mjini Kasulu.

Pichani juu ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Rungwe Mpya na Asante Nyerere katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo Kata ya Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
 Nape akikabidhi kadi kwa wanachama wapya.
 Baadhi ya Kadi zilizorejeshwa.
Mkuu wa Wilaya Kasulu, Danny Makanga akicheza ngoma wakati wa mapokezi hayo ya Nape Kijijini hapo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiweka jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kijiji cha Rungwe Mpya Wilayani Kasulu.
 Nape akiangalia jengo hilo la CCM
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Kata ya Asante Nyerere, Yohana Seif akizungumza katika mkutano wa hadhara mara baada ya kurejea CCM.
Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (katikati) akisalimiana na Diwani wa Kata ya Rungwe Mpya, Moris Mahabula wakati wa Mapokezi ya Katibu huyo. Kushoto ni Katibu wa Mwenezi wa Mkoa wa Kigoma, Zubery Mabie.
Akina mama wakishangilia ujio wa Nape kijiji cha Rungwe Mpya.
Nape akiwa na Mjumbe wa NEC, Kasulu, Daniel Nsanzugwanko.
Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Kigoma, Zubery Mabie, Mjumbe wa NEC Kasulu, Daniel Nsanzugwanko, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu wakisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa wajumbe wa Shina wa CCM Kasulu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisikiliza hoja mbalimbali za wajumbe hao.
Wajumbe hao wakifuatilia kikao hicho na Katibu wa Itikadi na Uenezi.
Wanachama wakila Kiapo cha CCM Kata ya Rungwe Mpya.
Burudani ya ngoma kutoka kikundi cha akina mama.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages