Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi
baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, leo. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza
masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali
waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kusalimisha hati ya
kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama na
kuripoti kwa msajili kila mwezi. Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba. Picha na Habari Mseto Blog
Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu
amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni
mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda
mrefu sana.
Lulu akitokwa na machozi ya furaha
Lulu akiingia kwenye gari
---
Baada ya jana kushindikana kwa sababu zisizo zuilika hatimaye msanii
maarufu Elizbeth 'Lulu' Michael ametoka kwa dhamana baada ya kutimiza
masharti yote ya dhamana yake yaliyo tolewa na mahakama kuu.
Mara baada yakutoka Lulu alieyeonekana akiwa mwenye majonizi na furaha
kiasi aliomba watanzania wote wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi
yake bado inaendela. Ali washukuru watu wote waliokuwa pamoja nae katika
mkasa huuu amabao bado unamzunguka na pia alimshukuru Mwenyezi Mungu
kwa kuwa pamoja nae katika kipindi chote cha matatizo yanayo mkabili
Wakili wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza
kwasababu case bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe
tarehe ya Lulu kurudi mahakamani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)