JK AZINDUA MIRADI MIWILI MIKUBWA WILAYANI IGUNGA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JK AZINDUA MIRADI MIWILI MIKUBWA WILAYANI IGUNGA LEO


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo la Mbutu,Wilayani Igunga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa Chujio la maji safi kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi zaidi ya asilimia 70 wa mji huo watapata maji safi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mashine ya kuchimbia mashimo ya nguzo  za daraja kabla ya kwenda kukata utepe kwa kuashiria kuzindua ujenzi  daraja la Mbutu,Wilayani Igunga leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale  (alieshika maiki) akumuonyesha Rais Kikwete ramani  ya Mradi wa Ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo la Mbutu,Wilayani Igunga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kutoa ushauri kwa kundi la vijana 10  ambao baada ya kumaliza chuo kikuu wamejikusanya na kuunda kikundi cha ujasiriamali mjini Igunga wakijishugulisha na Kilimo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua sehemu ya vyanzo vya mradi mpya wa maji  safi kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia 70 wa  mji huo watapata maji safi
Wananchi wakivuka katika sehemu itayojengwa daraja la kisasa eneo la Mbutu,Igunga Mkoani Tabora ambao ujenzi wake umezinduliwa leo na Rais  Jakaya Mrisho Kikwete, hatua ambayo itatatua kabisa tatizo la  miundombinu.PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages