Mmoja wa
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Andrew Chenge akiwasilisha
maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba leo Januari 7, 2013 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akifafanua jambo kuhusu
mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wananchi kwa viongozi wa Chama cha
Wananchi (CUF) waliofika katika ofisi za Tume kuwasilisha maoni ya chama
hicho kuhusu Katiba Mpya leo Januari 7, 2013:. Viongozi hao pia walipata fursa ya
kutembelea Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) na Kitengo cha Utafiti.
Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na kushoto ni
Mwenyekiti wa CUF Prof. Lipumba.
Mmoja wa Viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya
chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam.
Wajumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed
Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.
Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu
Katiba Mpya mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7,
2013) katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa
Tume Jaji Joseph Warioba na kulia kwa Prof. Lipumba ni Katibu wa Tume
Assaa Rashid.
Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba katika picha ya pamoja
na Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Mwenyekiti wao
Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya chama hicho kuwasilisha maoni yake
kuhusu Katiba Mpya kwa Tume jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)