WANANCHI WA VIJIJI JIRANI NA SHAMBA LA MUWEKEZAJI EPHATA MINISTRY WILAYANI SUMBAWANGA WATAKIWA KUWA NA SUBIRA NA UTULIVU WAKATI HUU SERIKALI INAPOTAFUTA SULUHU YA MGOGORO KATI YAO NA MUWEKEZAJI HUYO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANANCHI WA VIJIJI JIRANI NA SHAMBA LA MUWEKEZAJI EPHATA MINISTRY WILAYANI SUMBAWANGA WATAKIWA KUWA NA SUBIRA NA UTULIVU WAKATI HUU SERIKALI INAPOTAFUTA SULUHU YA MGOGORO KATI YAO NA MUWEKEZAJI HUYO


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ulinji kata ya Mollo ambao kijiji chao pamoja na vijiji vingine vya jirani vinavyozunguka shamba la Malonje linalomilikiwa na muwekezaji Ephata Ministry kwa muda mrefu sasa wamekuwa na mgogoro na muwekezaji huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa pamoja na mambo mengine muwekezaji huyo huwanyanyasa wananchi wanaopita kwenye maeneo yake
Wananchi wa Kijiji cha Ulinji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa makini. Mkuu huyo wa Mkoa alilzaimika kuongea na wananchi hao na kuwaeleza nia ya Serikali kumaliza mgogoro huo ili kuweka hali ya amani na utulivu katika eneo hilo ambalo siku za karibuni baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo walijichukulia sheria mkoanoni na kuchoma matrekta mawili na kuharibu moja ya nyumba ya muwekzaji huyo na kuiba mahindi. Watumiwa wa sakata hilo wapo mikononi mwa polisi na hatua nyingine za kisheria zinaendelea.  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Skaungu katika Kata ya Msandamuungano mjini Sumbawanga ambao pia kijiji chao kinapakana na shamba la muwekezaji huyo kuwapa mrejesho wa kikao cha dharura cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichojadili mgogoro kati yao na muwekezaji. Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Msandamuungano Kijiji cha Skaungu kilipimwa na kupatiwa hati ambapo inaonekana pia kuwa shamba la muwekzaji huyo lenye ukubwa wa hekta 1,000 limemega sehemu ya kijiji hicho. Mkuu huyo wa Mkoa alisema jambo hilo limesababishwa na upimaji wa aina mbili, moja ukiwa wa Wizara na mwingine kupitia ubinafsishaji wa Halmashauri uliopelekea kukosekana mawasiliano. Hata hivyo kamati imeshauri eneo la Kijiji libaki kama lilivyo na muwekezaji aridhie ili amani na utulivu iweze kupatikana katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwachagua watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwenda kupata chanjo ya minyoo na vitamin A katika kijiji cha Skaungu alipofanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho kuwapa mrejesho kama alivyowaahidi hapo awali kuhusu hatua Mkoa uliyofikia ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao na muwekezaji Ephata Ministry katika shamba la Malonje. Katika mkutano huo alihamasisha pia kilimo bora, elimu, afya kwa ujumla na mpango wa ONYARU "Ondoa Nyasi Rukwa" weka bati.
Ziara za Mkuu wa Mkoa wa Rukwa zinaenda sambamba na zoezi la chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto walio chini ya miaka mitano (5), Katika kijiji cha Skaungu watoto zaidi ya mia 300 walipatiwa chanjo hiyo.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria Mkutano huo, Pembeni kwenye gari ya maslaba mwekundu zoezi la chanjo likiendelea.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com

Pia kumekuwepo na malalamiko kuuwa Muwekezaji huyo anaenda kinyume na mkataba wake wa kufuga na badala yake amejikita zaidi kwenye kilimo. Wananchi pia wanalalamika kutokuwa na maeneo ya kulima kutokana na eneo kubwa kumiliki muwekezaji huyo. Kwa upande wa muwekezaji anadai kuwa wananchi wa vijiji hivyo jirani hufanya uharibifu shambani kwake pamoja na wizi. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alilazimika kuunda kamati kuchunguza mgogoro huo ambapo ilikabidhi taarifa yake na kusomwa hivi karibuni kwenye kikao cha dharura cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) na kutoa mapendekezo yake. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi hao kuwa watulivu kwani mgogoro huo unaenedelea kutafutiwa suluhu ambapo kamati ya ushauri ya Mkoa imeshatoa mapendekezo yake kwa kushirikiana na kamati aliyoiunda ambapo muhtasari wa kikao hicho utapelekwa katika wizara husika na Serikali ambayo italiangalia suala hilo na kuweza kulitafutia ufumbuzi. 

 "Ninayosema hapa leo sio maamuzi ya mwisho bali kwa ngazi ya Mkoa tumeshamaliza sasa tunaipeleka ngazi ya juu ambayo ni Wizara na Serikali kwa ajili ya maamuzi zaidi" alisema Injinia Manyanya.  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages