Sasa imezinduliwa rasmi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akikata utepe kuzindua rasmi taarifa ya hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kushoto) Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot (wa tatu kulia), Afisa Mwakilishi wa UNEP Tanzania Clara Makenya (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava ( wa kwanza kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema katika Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) uliofanyika mjini Kampala Julai 2002, ulibaini kuwa ukosefu wa taarifa za hali ya mazingira katika bara la Afrika ni moja ya sababu zinazochangia mipango duni ya usimamizi wa shughuli za maendeleo na utekelezaji Mikataba ya Kimataifa ya utunzaji mazingira.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam akisema Tanzania ni moja ya nchi zinazotekeleza program ya mtandao wa taarifa za hali ya mazingira yaani “Africa Environmental Information Network (AEIN) chini ya ufadhili wa Shirika la Mpango wa Mazingira Duniani (UNEP).
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot akizungumza kabla Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa hajazindua Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema taarifa hiyo ina mapendekezo makuu 12 na kutoa wito kwa serikali ya Tanzania kutafakari kila pendekezo sambamba na kuzitumia taarifa za kimazingira kwa manufaa ya taifa.
Amesema
kutokana na hali hiyo AMCEN iliiomba UNEP wafadhili program ya Afrika
ya Mtandao wa Hali ya Mazingira (Africa Environmental Information
Network) ili kuongeza uwezo wa nchi za Afrika wa kuwa na Taarifa za Hali
ya Mazingira na Mtandao wa Habari baina ya nchi za Afrika.
Mh.
Huvisa ameweka wazi kuwa taarifa hiyo imekamilika na iko tayari kwa
ajili ya utekelezaji, na kuwa taarifa hiyo imeezea Historia ya jiji la
Dar es Salaam, Jiografia na Fiziolojia yake, suala la uchumi Jamii,
Sera, Sheria na Mfumo wa Utawala Kimazingira, Usimamizi wa Rasilimali ya
Ardhi, Rasilimali Maji, Madini na Nishati, Usimamizi wa Taka na Usafi
wa Mazingira, Uchafuzi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi. Picha
zote na Mo Blog.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)