Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist
Ndikilo alipokuwa akifungua Mkutano wa RCC tarehe 14 Dec. 2012 Kwenye
Ukumbiwa Chuo cha Benki Mwanza
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Bibi Isabela Marick akisoma Muhtasari wa kikao kilichopita cha RCC.
Mada kutoka Mamlaka ya Usuluhishi na Upatanishi kuhusu masuala ya kazi nayo iliwasilishwa.
Mhe. Mbunge Ndassa wa Jimbo la Sumve akichangia moja ya mada kwenye Mkutano wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa RCC wakiwa wamesimama, kukumbuka kifo cha aliye kuwa Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Mwanza kabala
--
Na: Atleya Kuni- Mwanza.
Kikao cha kamati cha Ushauri cha Mkoa wa Mwanza (RCC), mwishoni
mwa juma hili wamekutana katika Ukumbiwa Chuo cha Benki jiji Mwanza
nakujadili mambo kadha wa kadha yahusuyo maendeleo ya Mkoa Mwanza,
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mokoa wa Mwanza Eng. Evaristi Ndikilo,
Alisema lengo la kikao hicho ilikuwa kutahmini ni kwa jinsi gani
wameweza kutekeleza yale yote walio azimia katika kikao kilichopita cha
tarehe 03 June 2012.
Sambamba na kuangalia mambo mengine Mkuu wa Mkoa hakuacha
kuendelea kuhubiri suala la Amani, alisema mtu anapo fikiria kuanzisha
vurugu ajiulize anaanzisha vurugu kwa manufaa ya nani kwani tunapokuwa
na vurugu hata shughuli za maendeleo haziwezi kufanyika kwa ufasaha.
Alihimiza juu ya kila halmashauri kuongeza vyumba vya Maabara kwa
kila shule ilikufanya wanafunzi kupenda masoma ya sayansi, alisema kila
Shule ihakikishe inajenga maabara tatu za sayansi yaani Baiolojia,
Fizikia na Chemistry.
Kwa upande mwingine Mkuu huyo wa Mkoa alihimiza Ufugaji nyuki,
Alisema suala la ufugaji nyuki halihitaji Mtaji Mkubwa kama wengine
wanvyo fikiria, bali unapokuwa na Msitu tu basi nyuki wenyewe watakuja
kuwekeza hapo, anachopaswa kufanya nikuandaa mizinga yako basi nyuki
watakuja kuingia lakini pia tutakapofuga nyuki itasaidia katika utunzaji
wa Mazingira.
Kufuatia tishio la njaa kwa baadhi ya Wilaya za MKoa huo Mkuu huyo
wa Mkoa aliwahimiza wakulima na Viongozi wa Halmashauri kuhakikisha
wanawahiza wakulima kutilia mkazo katika kilimo cha Mtama, kwani
kitasidia sana katika kuepukana na njaa.
Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wa Kikao hicho
walipendekeza, Maghala ya Chakula yaliopo Wilayani Kwimba, yatumiwe na
Serikali katika kuhakikisha yanakuwa ni sehemu mojawapo yakuhifadhia
chakula cha Njaa, na kuacha kutegemea Bohari ya Shinyanga pekee kwani
Imekuwa na usumbufu sana pindi njaa inapotokea.
Katika kikao hicho mada mbalimbali ziliwasilishwa, mada hizo ni
pamoja na Hali ya kilimo na muelekeo wa Msimu wa ulimaji na upandaji,
ambapo mtoa Mada katika mada hiyo, katibu Tawala Msaidizi wa Uchumi Bw.
Ndaro Kulwijira alisema kwa Mkoa wa Mwanza Msimu wa Kilimo huanza Mwezi
wa Nane hivyo ni vema wakulima wakalijua hilo na wakaanza maandalizi ya
mapema katika kilimo.
Kwa uapande wake Afisa Mipango wa Sekretariti wa Mkoa wa Mwanza
Matia Levi, mabye alitoa mada juu ya zozi la Sensa, alisema kwaujumla
zozi hilo katika MKoa wa Mwanza lilienda vizuri, nakwamba
Wananchiwasubiri kusikia Matokeo yatakayo tolewa na Rais wa Jamuhuri
mwishoni mwa Mwezi Desemba.
Akifunga mkutano huo, Mkuu wa MKoa wa Mwanza ambaye pia ndiye
Mwenyekiti wa Kikao hicho, alionya baadhi ya wajumbe wanao kimbia
kuhudhuria kikao hicho na akasema kwamba kama kuna mtu anashindwa
kuhudhuria vikao halali namna hii, basi kuna kila haja yakuangalia kwa
upya nakutahmini sheria zinataka nini, Ndugu zangu haiwezekani mtu tu
kwa sababu zake aache kuhdhuria Vikao hivi vya Kisheria tena bila hata
ya taarifa halafu kesho na kesho kutwa aje atusumbe kwamba haelewi
kilicho jadiliwa.
Akashauri pengine kanuni zipitiwe na
Sheria ziangaliwe kwa upya ili
kama ni hatua za kinidhamu dhidi ya mtu huyo ziweze kuchukuliwa RCC
ndicho kikao kikubwa kabisa cha maamuzi katika ngazi ya mkoa na
kipo kwamujibu wa sheria namba 19 ya mwaka 1997 juu ya uanzishaji wa
Sekretarieti za Mikoa na kuhuishwa na tangazo la Novemba 2011 lililo
sainiwa na Mhe. Rais.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)