TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 29/12/2012
Chama cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati
(ECAPBA) kimepata nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Gaudence Lyimo kuomba kihamie Arusha ili
kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki, EAC”
Rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya
kuwa ECAPBA itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA
ina makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Juhudi za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na
kukuza utalii katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa
ECAPBA kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
Uamuzi huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama wa ECAPBA bw. Daudi Chikwanje ambaye ndiye
Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi!
Nchi ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia,
Ethiopia, Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na Sudan.
ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao
unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi Afrika.
Imetumwa na:
Onesmo Ngowi
Rais, ECAPBA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)