MKUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO LEO

Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwan Kikwete akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na changamoto zinazokabili chama hicho.
Waandishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi unaofanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
Mtaalam wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika mkutano huo
Kutoka kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani .PICHA NA FULLSHANGWEBLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages