WAHITIMU WATAKIWA KUWA WAADILIFU MARA WATAKAPOANZA KUTUMIKIA TAIFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAHITIMU WATAKIWA KUWA WAADILIFU MARA WATAKAPOANZA KUTUMIKIA TAIFA

BARAZA la Chuo cha Uongozi la Azania limewataka wahitimu wa chuo hicho kwenda kulitumikia Taifa kwa uadilifu ili kujijengea misingi ya kuwa viongozi bora miongoni mwa jamii.

 Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elias Issangya, wakati Mahafali ya tano ya Chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 364 walihitimu katika ngazi za stashahada za sheria na Uhasibu.
 
Alisema ili mtu aweze kuwa mfano kwa kuitwa kiongozi bora, anapaswa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya uadilifu ya kazi, itakayomjengea heshima ndani ya jamii husika kinyume na misingi hiyo, ni sawa na kujivunjia heshima katika jamii.
 
Kwa wahitimu wa sheria, Isangya aliwataka kuhakikisha wanatoa haki bila ya upendeleo kwa yeyote kwa lengo la kulinda misingi ya haki.
 
“Najua mpo mtakaokwenda kuongoza katika vyombo vya sheria, wajibu wenu mkiwa katika maeneo hayo ni kusimamia masuala yote kikamilifu mkizingatia misingi ya haki” alisema.
 
Aidha, aliwataka wahitimu wa fani a ya Uhasibu kuhakikisha  wanajiepusha na tamaa pindi wawapo kazini ili kujijengea sifa katika kazi hiyo.
 
Alisema ni wajibu wa kila mmoja kutambua kuwa heshima katika kazi ndiyo misingi ya maendeleo katika taifa lolote likiwemo la Tanzania.
 
Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 364 wamehitimu katika ngazi ya stashahada na cheti za fani ya uhasibu na sheria

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages