BARAZA
la Chuo cha Uongozi la Azania limewataka wahitimu wa chuo hicho kwenda
kulitumikia Taifa kwa uadilifu ili kujijengea misingi ya kuwa viongozi
bora miongoni mwa jamii.
Wito huo umetolewa jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elias Issangya,
wakati Mahafali ya tano ya Chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 364
walihitimu katika ngazi za stashahada za sheria na Uhasibu.
Alisema ili mtu aweze kuwa mfano
kwa kuitwa kiongozi bora, anapaswa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya
uadilifu ya kazi, itakayomjengea heshima ndani ya jamii husika kinyume
na misingi hiyo, ni sawa na kujivunjia heshima katika jamii.
Kwa wahitimu wa sheria, Isangya
aliwataka kuhakikisha wanatoa haki bila ya upendeleo kwa yeyote kwa
lengo la kulinda misingi ya haki.
“Najua mpo mtakaokwenda kuongoza
katika vyombo vya sheria, wajibu wenu mkiwa katika maeneo hayo ni
kusimamia masuala yote kikamilifu mkizingatia misingi ya haki” alisema.
Aidha, aliwataka wahitimu wa
fani a ya Uhasibu kuhakikisha wanajiepusha na tamaa pindi wawapo kazini
ili kujijengea sifa katika kazi hiyo.
Alisema ni wajibu wa kila mmoja
kutambua kuwa heshima katika kazi ndiyo misingi ya maendeleo katika
taifa lolote likiwemo la Tanzania.
Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 364 wamehitimu katika ngazi ya stashahada na cheti za fani ya uhasibu na sheria
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)