Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe, wakati alipowasili
katika hafla ya chakula cha jioni katika yake, Balozi na maaofisa wa
Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na maofisa wa ubalozi wa Tanzania
nchini Uingereza ili kuagana na kutathimini mapungufu na mafanikio ya
ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya dunia ya utalii World Treavel
Market (WTM) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini
Uingereza, ambapo zaidi ya makampuni 55 yanayouza na kutangaza utalii wa
Tanzania yalishiriki katika maonyesho hayo, maonyesho hayo hufanyika
kila mwaka eneo la Excel jijini London.
Balozi Khamis Kagasheki aliitaka
Bodi ya Utalii Tanzania kuongeza juhudi zaidi ili kuleta mafanikio zaidi
katika maonyesho hayo na mengine na kuongeza idadi ya watalii kufikia
milioni moja kwa mwaka, Tanzania ikijipanga vizuri na kutangaza vivutio
vyake zaidi duniani inaweza kupata mafanikio zaidi katika utalii na
kuongeza zaidi mapato yake ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi kupitia
sekta ya utalii.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika hafla
hiyo ambapo aliwashukuru maofisa kutoka Bodi ya Utalii na Taasisi zake
pamoja na makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo kwa maandalizi
mazuri katika ushiriki huo, lakini pia akaagiza kuangalia changamoto na
kuzifanyia kazi ili kuboresha zaidi ushiriki wa Tanzania katika
maonyesho yajayo na mengine yanayoweza kufanyika katika nchi zingine,
kulia katika picha ni Balozi Peter Kallaghe na kulia ni Mama Balozi
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe akizungumza katika
hafla hiyo kulia ni Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili na
Utalii.
Baadhi
ya maofisa waliohudhuria katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Dkt.
Wegoro kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha , Devotha Mdachi
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Balozi mdogo wa
Tanzania nchini Uingereza Mh. Kilumanga na Mkurugenzi wa Kituo cha
Biashara cha Tanzania ubalozini Bw. Kashangwa.
Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Meena wa pili kutoka
kushoto akiwa pamoja na maofisa kutoka TANAPA, Mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro na Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii
Balozi Khamis Kagasheki hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza
katika hafla hiyo.
Ofisa
Habari wa TANAPA Bw. Shelutete kulia akiwa na Maofisa wa Kituo cha
biashari cha Tanzania nchini Uingereza katikati ni Dilunga na kushoto ni
Mohamed
Wadau
wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kufungwa rasmi kwa
maonyesho hayo kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB) Bw, Geofrey Meena, Mdau Angela Msangi kutoka Shirika la Utangazaji
TBC, Juma Mabakila kutoka Jambo Concerpt na Mama Juma Pinto
Mdau
Hafsa Omary kulia akiwa na wadau wengine watanzania wanaoishi nchini
Uingereza ambao walihudumu katika banda la Tanzania wakati wote wa
maonyesho hayo.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza
mara baada ya kufungwa kwa maonyesho hayo yaliomaliziki mwishoni mwa
wiki, aliyeshika kinasa sauti ni Hafsa Omary aliyewahi kufanya mazoezi
ya mafunzo ya uadhishi wa habari TBC hapa akikumbushia enzi zake.
Mh.
James Lembeli Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Maliasili, Utalii
na Ardhi akitoa machache mara baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo
wakati akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa TBC nchini Uingereza,
ambapo aliiomba bodi ya utalii kufanya jitihada za maksudi
kuwahamasisha na kuongeza idadi ya washiriki wazawa wa Tanzania katika
maonyesho hayo
Nami
nikapata japo picha moja na mdau Hafsa Omary mara baada ya kukamizika
kwa kazi nzima ya kuripoti matukio ya maonyesho hayo yaliyomaliziki
mwishoni mwa wiki iliyopita jijini London nchini Uingereza.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kulia akimsikiliza
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maliasili, Utalii na Ardhi
wakati alipokuwa kichangia mazungumzo katika hafla ya chakula cha jioni
baada ya kumalizika kwa maonyesho ya WTM nchini Uingereza mwishoni mwa
wiki iliyopita, katikati ni Balozi wa Tanzania nchini humo Balozi Peter
Kallaghe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)