Balozi wa Japan Mr. Masaki Akodo
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki
Okada kesho anataraji kutia saini makubalino ya msaada wa fedha kiasi cha
shilingi Milioni 380 kwaajili ya miradi miwili ya ujenzi wa bweni La
Wasichana pamoja na Shule ya watoto wenye ulemavu katika mikoa ya Lindi na
Mtwara.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na
Ubalozi huo jijini Dar es Salaam, inasemakuwa miradi hiyo ni upanuzi wa
shule ya wenye ulemavu Dinyecha Wilayani Mtwara utakao gharimu zaidi ya
shilingi Milioni 192 na
ujenzi wa bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu
shilingi
Milioni 188.
Miradi hiyo miwili
inasimamiwa na taasisi za Tanzania Life Improvement Association (TALIA) ya Mtwara na Women in
Social Entrepreneurship (WISE) ya mjini Lindi.
Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umekuwa
ukichangia fedha katika miradi mbalimbali ya Maendeleo katika sekta ya Afya,
elimu na maji tangu mwaka 1991 ambapo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita
mikoa ya Lindi na Mtwara imepatiwa msaada katika miradi 71 iliyogharimu dola za
kimarekani 6,135,418 sawa na shilingi Bilioni 9,614,629485.
Utiaji saini huo utafanyika katika ofisi
za mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mtwara kati ya saa 3 asubuhi na saa 5.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)