Mke
wa Waziri Mkuu Mana Tunu Pinda akitoa hotuba ya kufungua Maonyesho ya
Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini
Dar es Salaam ambapo amewahimiza wajasiriamali kujiunga katika ushirika
ili iwe rahisi kusaidiwa kupata mikopo, kutafuta masoko, kupanga bei
nzuri ya bidhaa zetu, kupata utaalam na teknolojia mpya. Kauli Mbiu ya
ya Maonyesho hayo mwaka huu ni “Msichana Amka, Ujasiriamali ni Ajira”.
Mama
Tunu Pinda akikata utepe kuzindua Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi wa
Maendeleo ya Wanawake Wajasiriamali (WEDEE) Ulio chini ya Shirika la
Kazi Duniani (WEDEE) wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Wanawake
wajasiriamali ya MOWE yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Mama Pinda akipokea vitabu toka kwa Noreen Toroka (wa pili kulia) na Hopolang Phororo wa ILO.
Mama
Tunu Pinda akisoma kwa furaha kitini cha mafunzo ya Wajasiriamali baada
ya kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Hopolang Phororo
na Noreen Toroka kutoka ILO.
Pichani Juu na Chini ni Mama Tunu Pinda akikagua baadhi ya mabanda na kujionea bidhaa mbalimbali katika maonyesho hayo.
Mama
Tunu Pinda akipokea kipeperushi kutoka kwa Noreen Toroka wa ILO
walioandaa maonyesho ya MOWE kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanawake na
Maendele0 (WAMA) iliyochini ya Mama Salma Kikwete.
Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja baada ya kufungua maonyesho ya MOWE 2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)