MABONDIA WA ZAMBIA WAWADUNDA WATANZANIA 4,1 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MABONDIA WA ZAMBIA WAWADUNDA WATANZANIA 4,1

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Masumbwi Mohamed Chibumbuli akiwa chini huku akihesabiwa baada ya kupata kichapo kutoka kwa bondia wa Zambia Mbachi Kaonga
Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Zinduka Entertaiment cha Temeke wakitoa burudani kabla ya mpambano wa Zambia na Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita
Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Zinduka Entertaiment cha Temeke wakitoa burudani kabla ya mpambano wa Zambia na Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita
Bondia Saidi Hofu wa Tanzania kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na bondia Caristo bwalia wa Zambia wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika mwishponi mwa wiki iliyopita
Bondia Mbachi Kaonga wa Zambia kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Mohamed Chimbumbui wa Tanzania Kaonga alishinda kwa point wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika mwishponi mwa wiki iliyopita
Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Joker Club Olec Aleksejev kulia akitunishiana misuri na bondia wa timu ya Taifa ya Masumbwi Said Hofu baada ya kumkabizi vifaa kwa ajili ya mchezo huo baasda ya kuibuka mcherzaji bora wa mashindano kati ya Zambia na Tanzania
Bondia Mohamed Chimbumbui wa Tanzania (aliyevaa nyekundu) akizuia ngumi nzito za Mbachi Kaonga wa Zambia kg 75
MABONDIA wa ngumi za Ridhaa wa Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita wamechezea kichapo baada ya kupigwa michezo minne kati ya mitano iliyochezwa  na mabondia toka Zambia kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Mapambano haya ambayo yalikuwa ni ya kirafiki ya kimataifa yanayojulikana na Shirikisho la ngumi za Ridhaa Duniani AIBA yenye raundi tatu ilishuhudia Said Hofu akifungua pazia (kg 49) kwa kupigwa kwa pointi na Caristo Bwalia toka Zambia


Mpambano wa pili kg 56 ulishuhudia Frank Nicolaus wa Tanzania akipigwa na Russel Mwamba wa Zambia kwa pointi pia.


Kg 60 ndipo mtanzania Ismail Galiatano alimshushia ngumi nzito nzito John Chimpwele wa Zambia na kusababisha kuchanika juu ya jicho na kutokwa damu nyingi ndipo mwamuzi alisimamisha mchezo na kumpa ushindi Ismail Galiatano.(RSC)


Mpambano wa nne kg 64 Mtanzania Kassim Hussein alipokea kipigo toka kwa  Charles Lumbwe kwa kupigwa kwa pointi.


Funga kazi kg 75 ikawa ndio usiseme maana Mohamed Chimbumbui alipigwa kwa TKO na Mbachi Kaonga wa Zambia baada ya kumsukumizia makonde mazito mazito na kushindwa kuyahimili na kujikuta akianguka kila mara.


Katibu wa Chama ngumi za ridhaa, Makore Mashaga alisema wamepoteza mpambano huo lakini anashukuru wamepata mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya ndano yanayotarajiwa kuanza Novemba 26 kwenye uwanja wa ndani wa taifa, jijini Dar es salaam.


Mabondia watanzania walisema kupigwa kwao kunatokana na maandalizi hafifu waliyopata na mashindano kuahirishwa mara kwa mara pia kuliwafanya morali kushuka.


Naye Katibu wa Ngumi za Ridhaa wa Zambia Lut. Kanali Man Muchimba amesema amefurahi kucheza na watanzania kwani wamepata mazoezi ya kuwasaidia kucheza mashindano ya kanda ya tano yatakayofanyika nchini kwao mapema Desemba.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages