Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision, Alfonse Kioko
(Kushoto) akipokea funguo za ndege mpya ya shirika hilo ya ATR 42-600
kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya ATR Filippo
Bagnato (kulia) wakati wa makabidhiano ya ndege hiyo yaliyofanyika
katika kituo cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya ATR Filippo Bagnato
(kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Precision
Alfonse Kioko (kulia) sehemu mbali mbali kwenye ndege mpya ya Kampuni
hiyo aina ya ATR 42-600 wakati wa makabidhiano ya ndege hiyo
yaliyofanyika katika kituo cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni
mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya ATR Filippo
Bagnato (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Precision
Alfonse Kioko (kulia) sehemu ya rubani kwenye ndege mpya ya Kampuni hiyo aina
ya ATR 42-600 wakati wa makabidhiano ya ndege hiyo yaliyofanyika katika kituo
cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa wiki. Picha na mpiga picha wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision, Alfonse Kioko (wa
kwanza) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuani ya Ndege ya ATR Filippo
Bagnato wakishuka kwenye ndege ATR 42-600 baada ya kuifanyia ukaguzi
kabla ya makabidhiano rasmi ya ndege hiyo yaliyofanyika katika kituo cha
ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Air, Alfonse Kioko
(kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Ndege ya ATR Filippo Bagnato (kulia) wakati wa makabidhiano ya ndege
hiyo yaliyofanyika katika kituo cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa
mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)
Na Mwandishi Wetu, Toulouse
SHIRIKA la
Ndege la Precision Air limekuwa shirika la kwanza kwenye bara ya Afrika
na dunia kwa ujumla kumiliki ndege ya kisasa aina ya ATR 42-600 baada
ya kukamilisha mchakato wa kununua ndege hiyo jana , Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya ndege ya ATR iliyopo jijini Toulouse , Ufaransa Filippo
Bagnato amesema.
Ndege hiyo
yenye thamani ya dola za kimarekani 16.4 milioni (Takribani shilingi
bilioni 26.24) ni ndege bora katika sekta ya usafiri wa anga duniani na
inazingatia usalama wa abiria kwa hali ya juu pamoja na kutoa aina mbali
mbali za burudani kwa abiria wanaosafiri.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhiwa ndege hiyo kwenye kiwanda cha ndege aina
ya ATR kilichopo jijini Toulouse, Ufaransa, mwishoni mwa wiki,
Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Alfonse Kioko alisema kuwa shirika
lake litawekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 100 kuongeza uwezo
pamoja na kutanua safari za shirika hilo katika kipindi cha miaka
michache ijayo.
Kioko alisema
kuwa ndege hiyo mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 50 iitatumika kupanua
safari ya shirika hilo ya Dar es Salaam – Kilimanjaro na kuongeza kuwa
safari hizo zitaanza rasmi ndani ya wiki mbili zijazo baada kuwasili kwa
ndege jijini Dar es Salaam wiki hii.
“Uwekezaji wa
dola milioni 100 utatuwezesha kuwa na jumla ya ndege mpya tano (nne
zikiwa ni ATR 42-600 na moja ikiwa ni ATR 72-600 pamoja na injini moja
mpya ya dharura) katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Ujio wa ndege
hizi utaongeza idadi ya ndege zetu za ATR kufikia 14 na kutuwezesha
kutoa huduma bora zenye uhakika,” alisema Kioko.
Awali
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ATR Filippo Bagnato alisema kuwa
Tanzania itaendelea kuwa soko muhimu la kampuni yake na kuongeza kuwa
atafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa mahusiano baina nchi hizo
yanaendelea kuimarika.
“Utoaji wa
ndege ya kwanza ya ATR 42-600 kwa Shirika la Precision ni swaala la
kihistoria katika bara la Afrika na duniani. Baada ya kukabidi ndege
hii Shirika la Ndege la Precision litakuwa miongoni mwa mashirika
mengine yanayotoa huduma bora na zenye uhakika.
“Kwa kutumia
ATR 42-600, Shirika la Precision itaendelea kujitanua kibiashara na
kukumbana na changamoto zilizopo katika sekta ya usafiri wa anga Afrika
na kutoa huduma zenye gharama nafuu,” alisema.
Kwa upande
wake Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Abubakar Kiroge wakati wa tukio hilo alisema kuwa uchunguzi katika
ndege hiyo umeshakamilika na kuongeza kuwa ndege hiyo inakidhi vigezo na
taratibu zote zinazotakiwa nchini Tanzania.
“Ndege hii
imekidhi vigezo vya kiusalama vinavyotakiwa. Mamlaka husika sasa ipo
tayari kuipatia Precision Air cheti cha kuwezesha ndege hiyo kutumika
nchini Tanzania. Ukweli ni kwamba ndege hii inazingatia usalama wa
abiria kwa haki ya juu,” alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)