Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk wamwanzo
kulia akimpa zawadi Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Conr ner
Baada ya kufanya Mazungumzo kuhusiana na mambo mbalimbali ya Michezo na
maendeleo ya Digital hapo Afisini kwake Kikwajuni Zanzibar.
-Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk
wamwanzo kulia akipeana mikono na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania
Diane Conr ner Baada ya kufanya Mazungumzo kuhusiana na mambo mbalimbali
ya Michezo na maendeleo ya Digital hapo Afisini kwake Kikwajuni
Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk wamwanzo
kulia akifanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane
Conr ner kuhusiana na mambo mbalimbali ya Michezo na maendeleo ya
Digital hapo Afisini kwake Kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo
wakimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diane Conr ner(hayupo
pichani)alipokutana na Waziri wa Habari wa Zanzibar hapo Afisini kwake
Kikwajuni.Picha na Yussuf Simai, Maelezo
-
Na: YUSSUF SIMAI.MAELEZO ZANZIBAR
-
Na: YUSSUF SIMAI.MAELEZO ZANZIBAR
Wazi wa Habari Utamaduni Utalii na
Michezo Said Ali Mbarouk amesema kuwa Zanzibar itahakikisha inaingia
katika Mfumo wa Digital kabla ya kufikia tarehe iliowekwa ili kwenda
sambamba na mabadiliko ya Ulimwengu. Waziri ameyasema hayo hapo Afisini
kwake Kikwajuni wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza
nchini Tanzania Diane Conrner .
Amesema licha ya Zanzibar kuingia
katika Mfumo wa Digital lakini inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa
pamoja na Vifaa na mafunzo kwa watendaji wake. Akizungumzia Sekta ya
Utalii Waziri Mbarouk alisema kuwa sekta hio inakua kwa kasi kubwa
kutokana na Wawekezaji Binafsi ambao huwekeza Zanzibar na kuweza
kuitangaza zaidi katika miji na Nchi tafauti.
Aidha amesema kuwa Serikali
inafarijika kuona Watalii wengi kutoka Uingereza na nchi nyengine za
Ulaya wanafika Zanzibar na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistiria
na vivutio vyengine vya Utalii vilivyopo nchini. Nae Balozi huyo Diane
Conrner ameipongeza Zanzibar kwa juhudi kubwa inazochukua katika
kuimarisha sekta ya utalii na kueleza matumaini yake kuwa sekta hiyo
itaendelea kuwa muhimili mkubwa wa uchumi.
Akizungumzia sekta ya michezo Balozi
Diane ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya ZanzÃbar kushiriki michezo
mbali mbali ikiwemo ya Kimataifa kwa vile michezo inatoa mchango
mkubwa katika kuitanga nchi kujulikana duniani kote.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)