NMB imekua mbele katika kuchangia
soka Tanzania, kwa miaka mitano mfululizo NMB imedhamini maendeleo ya
soka nchini.Udhamini huo uligawanyika katika kuendelza soka ya vijana na
timu ya Taifa. Kwa kwendeleza soka, Leo hii NMB imetangaza udhamini wa
shilingi milioni 15 kwa chama cha mchezo wa gofu Tanzania kwa ajili ya
maandalizi ya mashindano ya ‘NMB Nyerere Masters’
Mashindano ya Gofu ya NMB Nyerere
Masters yamekuwa yakichezwa kwa takribani miaka 12 kwa kumuenzi Baba wa
Taifa Mwl.Julius Nyerere. Hili ni shindano lenye hadhi katika nchi yetu.
Mashindano haya yanayotarajiwa
kuanza kutimua vumbi Oktoba 13-14 katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar
es Salaam,yamewavutia washiriki mia moja kutoka sehemu mbalimbali
nchini kama: Frank Roman na Abbas Adam kutoka klabu ya Moshi, Jimmy
Mollel na Nuru Mollel kutoka klabu ya Gymkhana Arusha. wengine ni
Sherida Chilipachi kutoka Morogoro na Fatma Makame kutoka Dar es Salaam.
Washiriki hao watashindania zawadi mbali mbali.
NMB ndio benki pekee ya kwanza
yenye matawi zaidi ya 140 na ATM zaidi ya 450 nchini, imekuwa kinara
katika ubunifu Tanzania kwa kuanzisha akaunti mpya nyingi na ndiyo
benki ya kipekee iliyopo takribani wilayani kwa asilimia 95 ya wilaya
nchini.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)