WAZIRI NYALANDU:MAANDALIZI YA MKUTANO WA AFRICA ENDELEVU UMEKAMILIKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI NYALANDU:MAANDALIZI YA MKUTANO WA AFRICA ENDELEVU UMEKAMILIKA

Naibu waziri wa maliasili na utalii Mhe.Lazaro Nyalandu akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es salaam kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mkutano mkuu wa kwanza wa Africa katika usimamizi wa utalii endelevu utakaofanyika mkoani Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC)kuanzia  tarehe 15-18 mwezi huu mwaka 2012.
Mkutano huo utajumuisha wajumbe 412 kutoka nchi 40 za Africa ambapo asilimia 59 ya wajumbe hao wanatoka Tanzania na asilimi 41 ya wajumbe wanatoka nchi nyingine za Africa mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa makamu wa Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Mh. Dr Mohamed Ghalib Bilal.wadau na watanzania kwa ujumla wametakiwa kwenda kuunyesha mali asili zao wanazotengeneza ili kujipatia soko na kujitangaza kupitia mkutano huo
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika  mkutano huo.PICHA NA PHILEMONI SOLOMON WA FULLSHANGWE

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages