Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Kidoti Tanzania Limited, Jokate Mwegelo akisisitiza jambo wakati wa
uzinduzi wa lebo yake ya Kidoti kwenye hotel ya Serena.
Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo wakionyesha staili tofauti za nywele zilizo tengenezwa na Kidoti
……………………………………….
Miss Tanzania namba mbili wa
mwaka 2006, Jokate Mwegelo amezindua rasmi lebo yake ya mitindo ya
nywele na nguo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Brand.
Jokate ambaye alianza
kujihusisha na masuala ya mitindo mwaka jana, alizindua lebo yake hiyo
kwenye hotel ya Serena na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa masuala ya
urembo, maonyesho ya mavazi, wanamitindo na wauzaji wa bidhaa hizo
kutoka kila kona ya jiji.
Alisema kuwa hatua ya kuamua
kuanzisha lebo hiyo ni moja ya mikakati yake ya kujitafutia fedha kama
mjasiliamali na lengo lake kubwa ni kutaka kusimama yeye mwenyewe katika
maisha bila ya kumtegemea mtu.
Alifafanua kuwa kabla ya
kuanzisha lebo na kampuni yake, alifanya utafiti wa hali ya juu,
kuhusiana na sekta hiyo na hatimaye kushiriki kwa mara ya kwanza katika
maonyesho ya mavazi ya Red Ribbon na sasa kuamua kwenda mbali zaidi kwa
kuingia katika fani ya nywele ambazo anatengeneza yeye mwenyewe.
Amesema kuwa mbali ya kushiriki
katika maonyesho mbali mbali, pia atakuwa anasambaza bidhaa zake za
nywele na nguo kwenye maduka mbali mbali ili kuwawezesha wananchi
kutumia bidhaa zake.
“Lengo langu kubwa ni kutawala
soko na kuwa milionea, hiyo ndiyo ndoto yangu pamoja na kuuza bidhaa
zangu hasa za nywele kuanzia shs 9,500 na 12,000. Nguo za Kidoti
zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi
vya urembo pamoja na vipodozi,” alisema Jokate.
Alisema kuwa msingi wa ubunifu
wake ni mchanganyiko wa kipekee wa kiini cha utamaduni wa Kiafrika
pamoja na mitindo ya kisasa ulimwenguni kwa ajili ya wanawake na wanaume
wa kisasa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)