Meli
kubwa yenye jina la FUKADA SALVAGE ikifanyakazi ya kuutandaza Waya Mpya
wa Umeme utakaotokea Tanzania Bara mpaka Zanzibar,hafla ya Uzinduzi wa
utandikaji wa Waya huo imefanyika huko Fumba Wilaya ya Magharibi Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANIZBAR
……………………………………………………
Na Ali Issa Maelzo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa
baraza la Mapinduzi Zanzibar DR Ali Muhamed Sheni amesema kukamilika
kwa jitihada za kulaza waya mpya wa umeme kutoka Fumba hadi Rasi
Kilomoni Dar es salaam wazanzibari wataondokana na tatizo la umeme wa
mgao linalo endelea hivi sasa.
Hayo ameyasema leo huko Fumba
wakati wa uzinduzi wa laini mpya ya umeme unao tarajiwa kumalizika
Disemba mwaka huu na kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ambao kwa
muda mrefu wanatumia nishati hiyo ya umeme wa mgao .
Amesema hali hiyo itamalizika
muda mfupi tu kwani umeme unaolazwa waya wake una megawati 100 ambao
utatosheleza mahitaji ya wazanzibari bila ya wasiwasi wowote.
Amesema hali hiyo ni ya
kufurahisha kwa wazanzibari kwani itaifanya Zanzibar kuendeleza shughuli
zake za kimaendeleo na kuinua uchumi zaidi bila upungufu wa huduma hiyo
.
“Waya uliopo una megawati 45
ambayo ni ndogo kwa matumizi ya wananchi lakini kukamilika kwa waya huu
mpya kutatosheleza mahitaji ya watu na katika mazingira ya kawaida si
rahisi umeme kukosekana ”ali sema Rais DR. Shein .
DR. Shein aliwasihi wananchi
kukubali kupokea na kutunza huduma hiyo kwa mashirikiano kuazia ngazi ya
shehia Wilaya Mikoa na Taifa kwa kuepuka kujenga ,kuchota mchanga na
kadhalika karibú na nguzo za umeme .
Aidha Rais huyo alishukuru
serikali ya Marekani kupitia shirika lake la changa moto za milenia (MCA
Compact) ,seriaki ya Japan kampuni ya VISCAS kwa matengenezo ya waya
huo na kuulaza baharini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)