Kiongozi
na mwimbaji wa bendi ya African Stars Lwiza Mbutu akiimba katika onesho
la bendi hiyo linalofanyika usiku huu kwenye klabu ya Mzalendo
Makumbusho jijini Dar es salaam ambapo kampuni ya ASET inazindua mpango
wake wa Twanga Facebook Fans Club unaokutanisha marafiki wa bendi hiyo
katika mawasiliano ya Mtandao lengo likiwa kusherehekea pamoja na wadau
wake mbalimbali wanaoisapoti bendi hiyo kupitia mitandao ya kijamii. Fullshangweblog iko ukumbini hapo
ikikumuvuzishia matukio haya moja kwa moja usiku huu kutoka Mzalendo Pub
Makumbusho jijini Dar es salaam.
Janet
Isinika mmoja wa waimbaji wakongwe katika bendi hiyo akifanya vitu
vyake jukwaani, siku moja aliwahi kuniambia unapokuwa mwanamuziki hata
kama una matatizo unatakiwa kusahau kila kitu unapokuwa jukwaani ili
kumburudisha na kumpa raha yule anayekutazama na kukuzikiliza.







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)