VIONGOZI SITA WA UAMSHO WATIWA MBARONI ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

VIONGOZI SITA WA UAMSHO WATIWA MBARONI ZANZIBAR


Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar, linawashikilia watu 65 wakiwemo viongozi sita wa kundi la Uamsho na Jumuiya ya Maimam  Zanzibar kwa tuhuma za kuchochea ghasia na vurugu zilizosababisha  vitendo vya uporaji wa mali na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Insptekta Mohammed Mhina,  amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa viongozi hao wa Jumuia mbili za  Kidini mjini Zanzibar, Polisi pia imewakamata watu wengine sita kwa  tuhuma za mauaji ya Askari Polisi.
Insepekta Mhina, amewataja viongozi waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimau Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmed(41) mkazi wa Mbuyuni na  Sheikhe Mselem Ali Mselem(52) wa Kwamtipura  ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar.
Wengine ni Sheikhe Azan Khalid Hamadi(48) wa Mtendeni, Hassan Bakari Suleiman(39) wa Tomondo na  Ustaadh Mussa Juma Issa(33), Suleiman Juma Suleimain(66) pamoja na Mussa Juma Issa(37) wote wa Makadara mjini Zanzibar.  
Inspekta Mhina amesema viongozi waliokamatwa ni wale walikuwa wakihojiwa na  Polisi tangu jana kwa lengo la kutafuta ukweli wa taarifa za kutekwa kwa Sheikhe Farid Hadi Ahmed kulikopelekea ghasia na uharibifu mbalimbali  kabla ya kujitokeza tena hadharani juzi.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kamamishina wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa amesema kuwa Jeshi la Polisi Visiwani humo linaendelea  na operesheni maalumu ya kuhakikisha kuwa kila aliyehusika katika ghasi  hizo anakamatwa na kukabili mkono wa sheria.
Akizungumzia maendeleo ya Upelelezi wa Kesi ya Kuuawa kwa Askari Polisi CPL Said  Abdarahaman Juma aliyeuawa usiku wa kuamkia Alhamis wiki iliyopita, Kamishna Mussa amesema Polisi wamefanikiwa kuwatia nguvuni watu sita kwa kuhusika na mauaji ya askari huyo.
Amesema hadi sasa Polisi inawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na  mauaji ya askari huyo ambapo watuhumiwa watatu walikamatwa mjini  Zanzibar na wengine watatu wamekamatwa mkoani Tanga.
Kamishna Mussa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Mohammed Said(35) wa Mwanyanya, Joli Gasuli(20) wa Vuga, Bakari Juma Yusufu(22) wa Mwembe  Makumbi  na Amour Rished(40) wa Bububu ambao walikamatwa mjini zanzibar siku ya kwanza lilipotokea tukio hilo.
Amewataja watuhumiwa wengine ambao wamekamatiwa Mkoani tanga na ambao tayari wamesharejeshwa Zanzibar kuwa ni  Ali salum Seif(21) na Abubakari Haji Mbarouk(32) pamoja na mdogo wake Mohammed Haji Mbarouk(21) wote wakazi wa  Ndagaa mkoa wa Kusini Unguja.

Kamishna Mussa amesema Polisi bado inaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na wale  watakaobainika kuhusika na mauaji ya askari huyo watafikishwa  mahakamani.
Amesema kwa ujumla tangu kukamatwa kwa viongozi hao hali ya usalama katika mji  wa Zanzibar imerejea upya na wananchi wameombwa kutoshabikia vitendo  vyovyote vile vitakavyoweza kupelekea uvynjifu wa amani.
Amewataka Wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kshiriki katika mikusanyiko na kuwa chanzo cha fujo na kwamba kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo  atashughulikiwa ipasavyo na mkono wa dola.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages