TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaka wananchi wa
Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani wanawataka katika Uchaguzi Mkuu
uliopangwa kufanyika Machi mwakani.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi kabisa kuamua
hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais aliyasema hayo leo Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya mazungumzo na
ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini Kenya uliomtembelea
Ikulu jijini Dar es salaam.
Ujumbe
huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru
Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa
chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama
cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi
ujao.
Wengine
katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe.
Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa
tiketi ya TNA Moses ole Sakuda na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli.
Rais
Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa
watakuwa washindani katika
kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na kusisitiza
kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa kiuchumi kwa
nchi za Afrika Mashariki.
Rais
Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa miongoni
mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia na vurugu
zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Rais
Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu hiyo ya
kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja kama ajali
iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake hawaitarajii kutokea katika
uchaguzi ujao.
Mwisho
Imetolewa na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
DAR ES SALAAM,
21 Oktoba, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)