Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Dar es Salaam
………………………………………………
Sikukuu ya Eid-El-Hajj itakuwa
siku ya tarehe 26 Ockoba mwaka huu ambapo kitaifa swala itafanyika
katika msikiti wa Vuchama wilayani Mwanga katika mkoa wa Kilimanjaro
ikifuatiwa na Baraza la Eid baada ya Swala.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Baraza Kuu la Waislam wa Tanzania (BAKWATA) mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa
sababu ya tarehe hiyo ni kutokana na siku hii ya leo kuwa mwezi pili,
Dhul-Hijja mwaka 1433 kwa mujibu wa kalenda ya Kiislam.
Aidha Mufti na Sheikh Mkuu wa
Tanzania Issa Bin Shaaban Simba amewataka Waislam wote nchini
kusherehekea kwa amani na utulivu sikukuu hiyo huku wakichunga mipaka ya
Allah (S.W).
Sheikh Shaaban Simba pia amewataka
waislamu kutii sheria za nchi na kuepukana na watu ambao wanataka
keleta tafrani za kidini hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)