Kampuni ya Megatrade Investment Limited yadhamini tamasha la Jambo Festival - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Kampuni ya Megatrade Investment Limited yadhamini tamasha la Jambo Festival

KUSHOTO ni meneja masoko wa kampuni ya Megatrade Investment Limited Bw.Goodluck Kway akimkabidhi hundi ya shilingi Milioni kumi Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jambo Festival ambaye pia ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Idea Afrika ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Bw.Augustine Namfua kwa ajili ya kudhamini Tamasha la Jambo Festival linalotarajiwa kufanyika tarehe 20 hadi 28 oktoba mwaka huu jijini Arusha. PICHA NA ASHURA MOHAMED ARUSHA .

Ashura Mohamed-Arusha
…………………………………………………..
KAMPUNI   ya Mega trade Investment  kupitia kinywaji chake cha K -Vant Gin wamekabithi kiasi cha hundi ya  shs 10 milioni kwa ajili ya kudhamini tamasha la kimataifa la Arusha la sanaa na utamaduni (Jambo Festival litakalofanyika oktoba 20 hadi 28 mwaka huu mkoani  Arusha.

 Akizungumza jana  wakati wa kukabithi hundi hiyo ,Meneja masoko wa Megatrade ,Bw.Goodluck Kway alisema kuwa tamasha hilo litahusisha wapenzi wa sanaa za mikono,maonyesho, ubunifu na utamaduni kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
 Bw.Kway alisema kuwa, baadhi ya faida nyingi zitakazopatikana kupitia tamasha hilo ni pamoja na kupandisha hadhi ya jiji la Arusha na kuliweka katika sura mpya na bora zaidi katika ramani ya ulimwengu , kuvutia na kukuza na kuendeleza utalii wa kawaida wa ndani na nje ya nchi.

 Alisema kuwa,tamasha hilo litawezesha  kutengeneza nafasi za ajira na biashara kwa vijana, wanawake na wafanyabiashara kwa ujumla kabla, wakati na baada ya tamasha, kutoa nafasi kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kushiriki na kufanya biashara katika tamasha hili na maonesho haya, kukuza na kuendeleza utalii wa kitamaduni lakini pia kutoa fursa adimu kwa jamii za Arusha na watanzania kwa ujumla kusherehekea sanaa na utamaduni wao wa asili.

 Kway alisema kuwa,  tamasha la Jambo linatarajiwa kuchukua takribani siku tisa likijumuisha shughuli na matukio mbalimbali.

 Naye Afisa Mkuu wa kampuni ya Idea Afrika ambao ndio waandaji  wa tamasha hilo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo,Bw.Augustine  Michael Namfua alisema kuwa,amefurahishwa sana na msaada huo kutoka Mega kwani ndio wadhamini wakuu.

 Namfua alisema kuwa,fedha hizo watazitumia kwa umakini uliokusudiwa katika kuhakikisha wamewasadia vijana mbalimbali katika kuibua vipaji vyao na hatimaye tamasha hilo kuwa la mafanikio makubwa.

 Aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kuja kuinua vipaji vyao katika tamasha hilo kwani hiyo ndiyo fursa pekee ya kuweza kujifunza kupitia kwa wasanii wenzao .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages