NMB YATOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WASHIRIKI WA MPANGO WA MAMA SHUJAA WA CHAKULA KATIKA KIJIJI CHA MAISHA PLUS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NMB YATOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WASHIRIKI WA MPANGO WA MAMA SHUJAA WA CHAKULA KATIKA KIJIJI CHA MAISHA PLUS

Mkurugenzi wa Maisha Plus,Masoud Kipanya (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB ,Imani Kajula (pili kulia) ,Mwakilishi wa Idara ya Kilimo wa NMB, Carol Nyangaro (wa pili kushoto) na Meneja wa Mikopo Midogo ya Biashara, Mashaga Changarawe.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB,Imani Kajula (kulia) akiwagawia jarida la NMB Financial Fitness baadhi ya wakinamama wa Mama Shujaa wa Chakula  katika kambi ya Maisha Plus, jarida hilo lina maelezo mengi yanayohusu uelewa wa matumizi ya fedha.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB ,Imani Kajula (kushoto) akiwasomea jarida la NMB Financial Fitness wakinamama  wa Mama Shujaa wa Chakula katika Kambi ya Maisha Plus,  jarida  hilo lina maelezo mengi yanayohusu matumizi mazuri ya fedha.
Meneja wa Mikopo Midogo ya Biashara, Mashaga Changarawe.akipata kinywaji kwenye kibuyu alipowatembelea wakinamama shujaa wa chakula katika kijiji cha Maisha Plus.

 ………………………………………………
NMB ikiwa wadhamini wakuu wa mpango wa mama shujaaa wa chakula, imewatembelea washiriki  wa mama shujaa wa chakula  katika kijiji i cha Maisha Plus  na kuwapa elimu ya kifedha kupitia mpango wa NMB Financial Fitness.

NMB kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha imepata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.

Vilevile, Washiriki hao walielimishwa kuhusu Mikopo Midogo na kati ya kibiashara pamoja na mikopo ya kilimo. NMB inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages