MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MFANYAKAZI WA OFISI YAKE, JIJINI DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MFANYAKAZI WA OFISI YAKE, JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, Jenkins Chochole Matulile, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani  kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Mama Mzazi wa marehemu, Jenkins Chochole Matulile, wakati alipofika nyumbani  kutoa pole na heshima za mwisho kutokana na msiba huo wa aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifnyika nyumbani kwa kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu,  Jenkins Chochole Matulile, aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani  kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo.
 Makamu akijumuika na waombolezaji.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages