Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akihudhuria Mkutano wa tano wa
Viongozi Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyia kwenye Ukumbi wa
Commonwealth wa Hotel ya Munyonyo jijini Kamapala jana. Wengine
kutoka kushoto ni Rais Paul Kagame wa Rwanda na Makamu wa Rais wa Sudan,
Haji Adamu Yusufu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia
Bilal wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kilele cha
maadhimisho ya Miaka50 ya Uhuru wa Uganda kwenye Uwanja wa Kololo,
jijini Kampala jana. Wengine kutoka kushoto ni Rais wa Somalia Hassan
Shekhe Mahamoud na Makamu Rais wa Sudan, Bwana Haji Adam Yusufu.
Rais
Yoweri Museveni wa Uganda akimkaribisha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye sherehe za
maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda zilizofanyika jana kwenye
Uwanja wa Kololo jijini Kampala,Uganda.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gaharib Bilal
(kulia) akibadilishana mawazo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati
wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 yaUhuru wa Uganda. Sherehe hizo
zimefanyika jana katika Uwanja wa Kololo jijini Kampala. Wanaoonekana
nyuma yao ni wake zao, Bibi Janneth Museveni (kulia) na Mama Zakia
Bilal.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)