Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akizungumza katika ibada maalum iliyofanyika
katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbagala na iliyohudhuriwa na maaskofu wa
kanisa hilo na kutoa pole kuhusiana na matukio ya kuchomwa moto makanisa ya
kikristo katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wamini wa Kanisa la KKKT wakiwa katika ibada
maalumiliyofanyika katika kanisa la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati
maaskofu wa kanisa hilo walipokutana na kutoa tamko kuhusu kuchomwa kwa
makanisa ya Kikristo katika eneo la Mbagala na waislamu
Kanisa la KKKT Mbagala lililofanyiwa uharibifu mkubwa pamoja na kuchomwa moto kwa vitu mbalimbali katika kanisa hilo
Baadhi ya vifaa vilivyochomwa
Maaskofu wa Kanisa la KKKT wakitembelea na kujionea hasara iliyopatika katika kanisa hilo baada ya kuchomwa moto
Baadhi ya waamini wa Kanisa la KKKT wakiangalia madhabau ya Kanisa lao baada ya kuchomwa
Polisi wakihakikisha usalama wa waamini wa Kanisa hilo wakati wa ibada yao.Picha zote na Habari Mseto Blog
DAR ES SALAAM, Tanzania
KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, limeonyeshwa
kushangazwa kwake na ukimya wa Serikali pamoja na vyombo vya dola wa kutochukua
hatua mapema za vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyokuwa vikitendeka.
Kanisa hilo pia limeeleza kusikitishwa kwake kwa
vitendo vya uchomaji wa makanisa wakieleza kuwa kilichotokea mbagala katika
wiki ya kuadhimisha siku ya baba wa Taifa ni kebehi si kwa baba wa Taifa bali
kwa watu waliokalia kiti chake.
Akizungumza wakati wa ibada maalum na kutoa
salaam za Maaskofu wa KKKT kwa Watanzania wote kuhusiana na matukio ya kuchoma
moto makanisa ya kikristo iliyofanyika kanisa la jimbo kuu kusini Mbagala, Askofu
Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, dk. Martin Shao,alisema kuwa wamekutana kwa
dhumuni la kuonyesha majonzi yao kwa vitendo vya uvunjifu wa amani walivyoviita
ni kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania.
Shao pia alisema kuwa madhumuni mengine ni
kupokea matumaini ya Tanzania mpya katika msiba wa wenye dini na wasio na dini.
Aidha alisema kuwa katika ujio wa maaskofu 19 kutoka
dayosisi mbalimbali za Tanzania hawakwenda Mbagala kuhukumu hata kama
hawakubaliani na waliokashifu dini za wenzao.
“Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na
wanaokashifu dini za wenzao,wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama
wanajituma wenyewe,hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini
wawe wmetumwa,kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao
binafsi ili kupata kisingizio cha kugombanisha madhehebu ya dini “alisema.
Pia alisema kuwa hawakubaliani na wanaochoma
makanisa na kuiba mali za kanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu kwani kisasi
cha dhambi wanamuachia mungu aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.
Askofu Shao alifananisha kuwa kilichotokea
Mbagala ni mateso ya kimbari ambayo mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema imezaa magugu
yanayozaa matunda machungu.
“Dalili za mateso ya kimbari zilianza kitambo na
hazikushughulikiwa na waliomrithi Bababa wa Taifa dalili hizo za uchochezi wa
wazi kuwa Taifa hili linaendeshwa na unaoitwa mfumo wa kristo,ubishi usio na
tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki
kushawishi na kugomea sensa”alisema
Pia alilaani matumizi mabaya ya baadhi ya vyombo
vya habari vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini huku
vikifumbiwa macho na vyombo vya dola.
“Uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa
mustakabali wa Taifa letu na kwa watanzania wote wawe wengi dhidi ya wachache
au wachache dhidi ya wengi”alisema
“Ni uvumilivu gani wakati tumeshuhudia makanisa
yakichomwa Zanzibar,Mwanza,Mdaula, Mto wa Mbu,Tunduru na
kwingineko,tumeshuhudia Wizara zikivamiwa,vituo vya polisi vikichomwa,uhai wa
viongozi wa dini ukutishwa,viongozi waliostaafu wakizabwa makofu hadharani,
watu hawa wavamie nini ili hatua kali zichukuliwe au wamuue nani ili iaminike
kuwa ni tishio kwa usalama wa Taifa letu?” alihoji.
Shao alisema kuwa uvumilivu wa wakristo
umetafsriwa kuwa unyonge na woga na kufafanua kuwa wanyonge na waoga hufika
wakatin wakasema basi pale wanapodhalilishwa kupita kiasi.
Naye Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki
na Pwani, Dk.Alex Malasusa, aliwataka wakristo kuwa watulivu na kufunga na
kuomba ikiwemo kuonyesha upendo.
Katika hatua nyingine kanisa la Faraja
International Gospel Church, limechomwa moto na watu wasiofahamika na
kusababisha hasara ya sh. Milioni 5.8.
Mchungaji wa kanisa hilo lililopo Yombo
Makangarawe,Peter Kusaga alisema kuwa watu hao walivamia majira ya saa 7 usiku
kabla ya kuokolewa na majirani na kuteketeza amplifaya,maiki kumi,mixer.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema,
aliwataka wananchi kuwa na subira na kueleza kuwa vitendo vya uchomaji wa
kanisa sheria lazima ichukue mkondo wake kwani hakun aliyejuu ya sheria.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)