Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Barnaba
Elias ‘Barnaba’ amewataka mashabiki wake na wapenzi wa muziki wa bongo fleva
wakae mkao wa kula kwaajili ya kibao chake kipya ambacho bado hajakipatia jina.
Akizungumzia kazi hiyo jijini Dar es Salaam, Barnaba alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho
ambacho anaamini kitakua gumzo kwa wapenzi wa kazi zake.
Alisema anamshukuru mungu kazi zake zinafanya
vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya
na anawaomba wasanii wenzie wafanye kazi ambazo zinaelimisha jamii.
“Unajua msanii ni kioo cha jamii, hivyo
tunatakiwa kufanya mambo ambayo yanaeleweka na kuelimisha jamii, naomba wapenzi
wangu make mkao wa kula,” alisema Barnaba.
Barnaba alishawahi kutamba na vibao vyake kama,
Nabembelezwa, Wrong Number, Magumegume na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri
katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)