Mwita, Naali waibuka vinara Rock City Marathon 2012 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mwita, Naali waibuka vinara Rock City Marathon 2012

 Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 497 walijitokeza kushiriki mashindano hayo. 
 Mwanariatha Copro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo. 
 Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
 Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
 Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza

MWANZA, Tanzania

MWANARIADHA  mahiri Copiro Mwita wa Mwanza na Mary Naaly wa Arusha, jana waliibuka vinara upande wa wanaume na wanawake, katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 ya ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.

Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume akitumia saa 1:04:02, huku Mary akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa 1:16:33, katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wanariadha 497 waliokimbia katika makundi matano.

Dotto Ikangaa kutoka Arusha aliibuka mshindi katika mbio za kilometa tano wanaume, akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili, huku Paul Elias kutota Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.

Rock City Marathon ni mbio zinazondaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa na NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Katika mbio hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa na msanii maarufu wa Tanzania Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK Wanaume, akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.          

Rais wa Shirikisho cha Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, licha ya kutoa onyo kwa wavamizi wa viwanja vya michezo, alionesha kuridhishwa nuratibu wa Rock City Marathon, huku akiongeza kuwa mbio hizi zimeweza kuibua vipaji vingi vya riadha ambayo vinahitaji kukuzwa.

“Nawashukuru sana waandaaji wa Rock City Marathon kwa kuweza kuandaa mashindano ambayo yameweza kutusaidia sisi wadau wa riadha kugundua vipaji vingi ambavyo tunavyo hapa nchini ambavyo vinahitaji kukuzwa,” alisema Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro.

“Hivyo basi natoa wito kwa makampuni, mashirika na hata serikali, kuweza kudhamini mashindano kama haya ambayo yanasaidia sana kuendeleza na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha ambao umeliletea sifa kubwa taifa letu huko nyuma,” alisisitiza Mtaka.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alisema Rock City Marathon imeonesha kuvuta hisia na kukubalika miongoni mwa washiriki, kutokana na kuhusisha mbio za ngazi zote; nusu marathon, kilometa tano, kilometa tatu kwa walemavu, kilometa tatu kwa wazee na kilometa mbili kwa watoto.

Washiriki kutoka mikoa mbali mbali nchini walishiriki Rock City Marathon 2012, pamoja na wageni kutoka nchi za India, Canada, Australia, Afrika Kusini, Rwanda, Kenya na Uganda, ambapo washindi wa pili wa mbio za kilometa 21, wanaume na wanawake walijishindia shilingi 900,000 kila mmoja. 

Washindi wa tatu kilometa 21 waliondoka na shilingi 700,000 kila mmoja na wa nne hadi wa 10 walizawadiwa shilingi 150,000 kila mmoja. Wale walioshika nafasi ya 11 hadi 25 waliondoka na kifuta jasho cha shilingi 100,000 kila mmoja kwa upane wa wanaume na wanawake.

Jeremiah Kinshuzi wa Mwanza alishinda mbio za kilometa tatu kwa wazee, huku Pascal Emanuel wa Kisese akishinda kwa watu wenye ulemavu na walizawadiwa shilingi 50,000 kila mmoja, shilingi 30,000 kwa washindi wa pili na washindi wa tatu wakijipatia shilingi 20,000.

Kwa upande wa watoto ambao walikimbia kilometa mbili, Idd Suguta wa Mara na Emma Imhoff wa Singida waliibuka washindi na kuzawadiwa shilingi 30,000 kila mmoja, huku washindi wa pili wakipata shilingi 20,000 na wa tatu 15,000 na  walioshika nafasi ya nne hadi 25 wakapata kifuta jasho cha shilingi 10,000 kila mmoja.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages