Familia ya Marehemu Emily Tilito
Maro ya Uru-Kishimundu inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu jamaa
na marafiki wote walioshiriki nasi katika kufanikisha mazishi ya mdogo
wetu marehemu Raymond Emily Maro aliyefariki dunia tarehe 2 Septemba
2012 na kuzikwa kijijini Uru Kishumundu tarehe 6 Septemba
2012.Mlijitolea kwa moyo wa pekee nasi tunasema tuliguswa sana na upendo
na ukarimu wenu Mungu awatuze kwa wema wenu.Shukrani za pekee ziwandee
madaktari na wauguzi wa Hospitali za Seliani na St.Thomas Arusha
waliofanya kazi kubwa kujitahidi kuokoa maisha ya marehemu.Pia tunatoa
shukrani kwa uongozi wa TRA Makao makuu Arusha na Namanga kwa
kufanikisha mazishi ya Marehemu.Tunawashukru pia Mapadri wote wa Parokia
ya Kishumundu kwa kuendesha misa ya Mazishi.
Tunapenda kuwaarifu ndugu,jamaa na
marafiki kuwa shughuli ya kumaliza msiba(Arobaini) itafanyika kijijini
Uru-Kishumundu Jumamosi tarehe 3 Novemba 2012.Wote mnakaribishwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)