Mh Balozi Kallaghe Akisaini kitabu cha wageni
Mh Balozi akiongea na wanajumuiya
Mh Balozi katika akipokea zawadi kutoka kwa wanajumuiya
Ustadhi akiongea machache wakati wa chakula
Mwenyekiti wa ZAWA Hassan Khamis akimfafanulia jambo Mh Balozi
Watoto wa Kasida wakisikiliza Hotuba ya Mh Balozi
Vijana wa Kasida wakitumbuiza
Mh Balozi akionyeshwa manzari tofuti ndani ya Jengo
Mh Balozi katika picha ya pamoja
----
Salam,
Siku ya Jumamosi tarehe
27.10.12 Mh Balozi wetu wa Tanzania hapa nchini Uingereza alishiriki
sherehe ya siku kuu ya Iddi iliyofanyika London mashariki. Sherehe hii
ya baraza la EID (IDDI) iliandaliwa na Jumuiya ya East African Education
Foundation wakishirikiana na Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK (ZAWA)
Wakati akitoa hotuba yake Mh Balozi Peter Kallaghe
ambaye ndio aliekua mgeni rasmi siku hii ya leo, alianza kwa kuwashukuru
kwa mualiko huu mzuri alioupata na kuwatakia kila kheri wale wote
waliofanikiwa kutekeleza HIJA kwa mwaka huu 2012. Aidha Mh Balozi
ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Ubalozi na Jumuiya
mbalimbali za Watanzania zilizopo nchini Uingereza na Ireland. Pia
alivutiwa na kuipongeza hatma ya East African Education Foundation
kuazimia kununua Jengo hili kwa ajili ya shughuli za kijamii na
wanajumuiya wote kwa ujumla.
Baada ya kumaliza hotuba yake Shekhe Nasssor Haroub
nae aliongea na wanajumuiya akitilia mkazo zaidi umuhimu wa Umoja na
mshikamano kama Uislamu unavyo sisitiza kupitia Ibada ya HIJA. Vilevile
vijana wa kasida walipata fursa ya kutumbuiza alipomaliza kuongea Shekhe
Nassor.
Mwishoni Balozi alifanya ziara fupi ya kukagua jengo
hili na kupata maelezo kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Jumuiya ili
kujua namna gani litakavyoweza kutumika mara baada ya hatua za ununuzi
zitakapo kamilika rasmi kwa gharama za paundi laki 6 (£600,000)
Asanteni,
Urban Pulse Creative
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)