WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DK HUSSEIN MWINYI AFANYA ZIARA TAASISI YA SARATANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DK HUSSEIN MWINYI AFANYA ZIARA TAASISI YA SARATANI

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi  akisalimiana na mmoja wa wagonjwa wa saratani waliolazwa katika wodi hospitalini hapo. Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Twalib Ngoma alisema hivi sasa watanzania 100 wanafariki kwa ugonjwa wa saratani na asilimia 35 ya ugonjwa huo unaweza kuzuilika.
 Mh. Dkt. Mwinyi akipata maelezo toka kwa mtaalam(hayupo pichani) wa mashine inayosaidia kuchanganya dawa za mionzi na kuchunguza wagonjwa mbalimbali ( Nuclear Medicine)iliyopo katika jengo jipya la hospitali ya Ocean Road.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika chumba cha mionzi. Idadi ya wagonjwa wa saratani  imeongezeka toka wagonjwa 2,000 mwaka 2002 hadi kufikia wagonjwa 5,000 hivi sasa.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road wakimsikiliza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwenye ukumbi wa Mkutano hospitalini hapo.Picha zote na Catherine Sungura-Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages