Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Chadema na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akionesha picha ya polisi wakizingira Ofisi ya Tawi
la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo, Mufindi iliyochapishwa na
gazeti la Tanzania Daima Jana
---
DAR ES SALAAM, Tanzania
CHAMA
cha Demokrasi na Maendelea (Chadema), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete
kuwasimamisha kazi vigogo wote wa Jeshi la Polisi, ambao wamekuwa
wakitoa taarifa mbalimbali za uongo kuhusu mauaji ya mwandishi Daudi
Mwangosi, ama awatake wajiuzuru nyadhifa zao, kupisha uchunguzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari
na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika, aliwataja vigogo hao wa polisi
kuwa ni Kamanda wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja na RPC wa Iringa,
Michael Kamuhanda
Wawili
hao kwa mujibu wa Mnyika, kwa nyakati tofauti walidai kuwa marehemu
alifikwa na mauti baada ya kuchoropoka kutoka kwa kundi la wafuasi wa
Chadema na kukimbilia mikononi mwa Polisi na ghafla kulitokea mlipuko wa
bomu la machozi uliosababisha kifo chake, jambo ambalo sio la kweli.
Mnyika alisema maneno hayo yanayotofautiana na kuyaita kuwa ni ya uongo ukizingatia kwamba picha mbalimbali zimeonesha ikiwemo waandishi waliokuwemo eneo la tukio kutoa ushuhuda wao.
Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi huyo alisema ipo haja ya vigogo hao kung’oka kupisha
uchunguzi, ili uweze kufanyika kwa haki na kuongeza kwamba Rais atumie
madaraka yake kuhakikisha askari saba wanaoonekana katika picha
'wakimshughulikia' marehemu kukamatwa haraka na kuhojiwa ni nani alifyatua
bunduki, kwa namna gani na vigogo gani walitoa amri hiyo.
Kwa
mujibu wa Mnyika, Polisi imekuwa na tabia ya kukamata raia wanaokuwa
eneo la tukio pindi kunapotokea mauaji kama hayo, hivyo ni wakati sasa
wa Polisi wanaoonekana katika picha wakimshambulia marehemu Mwangosi nao
kukamatwa.
Aidha
alilitaka Jeshi la Polisi nchini lisitumie vibaya fedha za walipa kodi
kwa kuchunguza nani alihusika na mauaji hayo wakati wauaji wanaonekana
wazi kwenye picha za aina tofauti, badala yake kinachotakiwa na wao
kuhojiwa nani aliwaamuru kufanya mauaji hayo ya kinyama.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)