WAKAZI WA MOROGORO WAFURAHIA VYA KUTOSHA SERENGETI FIESTA 2012 USIKU WA KUAMKIA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAKAZI WA MOROGORO WAFURAHIA VYA KUTOSHA SERENGETI FIESTA 2012 USIKU WA KUAMKIA LEO



Pichani kulia ni Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh Joel Bendera ambaye ni mgeni rasmi usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakati tamasha la Serengeti likiendelea kufanyika.
 Pichani mbele ni msanii Rich Mavoko akiliongoza kundi lake jukwaani
 Ommy Dimpoz pichani kati sambamba na kundi lake wakitumbuiza kwenye jukwaa la Fiesta
 Hapatoshi ndani ya uwanja wa jamhuri usiku,heka heka mwanzo mwisho.
 wakazi wa mji wa Morogoro walivyojitokeza kwenye tamasha la Fiesta
 Ni shughuli moja tu juu ya jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 
 Mkali wa R&B Ben Paul akiwaimbisha wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwa wingi usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Jamhuri.
Msanii wa bongofleva Linah akitumbuiza jukwaani
Msanii mahiri katika mahadhi ya Mduara AT akiduarika na mmoja wa densa wake jukwaani .
Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro,ambapo wakazi kibao wa mji huo (hawapo pichani) wamejitokeza kwa wingi.
Mmoja wa sanii chipukizi katika shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Ney Lee akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani
Pichani juu na chini ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dayna na kundi lake la Wakali wa Classic wakitumbuiza jukwaani
Mkali wa Supa Nyota,Jo Meka akikamua jukwaani.
Mkali wa kusugua mangoma,Dj Zero akifanya makamuzi yake.
Muziki ni hisia kama hivi.
Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka mjini Morogoro akitumbuiza usiku wa kuamkia leo kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012
Msanii chipukizi kutoka nyumba ya vipaji,THT,Alini Nipishe akiimba na shabiki wake jukwaani usiku wa kuamkia leo wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea.
Michael Jackson wa Morogoro akionesha umahiri wake kucheza nyimbo za The Wacko Jacko.
Wakazi wa Morogoro wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri,ambako ndiko tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea
Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka mjini Morogoro akiimba jukwaani.
Wadau mbalimbali wa tamasha la Fiesta wakifuatilia burudani mbalimbali zikiendelea
Morogoro kuna vijana wengi wenye vipaji,ambao kiukweli wameonesha vilivyo kwenye jukwaa la Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo.
Wadau wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri usiku wa kuamkia leo.
Ni burudani tu ndani ya muonekano mpya wa tamasha la serengeti fiesta 2012.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages