Kamati ya Redds Miss Tanzania
leo inatarajiwa kutembelea kambi ya Redd’s Temeke 2012, kubwa ni
kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na
Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.
Kamati hiyo itaongozwa na
Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na mshauri wa masuala ya
urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, katibu Bosco Majaliwa, Mkuu
wa Itifaki, Albert Makoye na mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta.
Shindano la Redd’s Miss Temeke,
linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA(SabaSaba Hall) na tiketi za
VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za City Sports Lounge
iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo
ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000 na pia waweza nunua
kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi laki 5.
Warembo hao ni Agness Goodluck,
Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana,
Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth
Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam
Ntakisivya na Esther Albert.
Mbali ya vinywaji vya Redd’s na Dodoma Wine, Miss Temeke pia imedhaminiwa na gazeti la Jambo Leo, katejoshy.blogspot.com,
Mariedo Boutique, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM,
Kitwe General Traders, Global Publishers na 88.4 Cloud’s FM.
Shindano hili litakuwa ni
miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata warembo
watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini kumtafuta
mrembo wa Redds Miss Tanzania kwa Mwaka huu.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)