Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania Anjela Shila (Kulia) akihojiwa na
mtangazaji wa Kituo cha Radio 5 cha mkoani Arusha Devid Rwenyagira
katika kipindi cha ‘Good Morning’ wakati wa kuutangaza Mradi wa Mapitio
ya Mfumo wa Utoaji Haki katika Mashauri ya Madai.
Mkuu
wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Bw. Jowika Kasunga akipokea
vipeperushi vinavyoelezea Mradi wa Mapitio ya Mfumo wa Utoaji Haki
katika Mashauri ya Madai Tanzania kutoka kwa Afisa Sheria Mkuu wa Tume
Anjela Shila ofisini kwake Wilayani Monduli mkoa wa Arusha.
Na Munir Shemweta, Arusha
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imeanza kuutangaza mradi wa Mapitio ya Mfumo wa Utoaji Haki katika Mashauri ya Madai nchini.
Katika
hatua hiyo Maafisa Sheria wa Tume wameenda mikoa sita ya Tanzania Bara
kwa ajili ya kuzungumzia mradi huo kupitia vituo vya Radio vilivyopo
katika mikoa husika.
Mbali
na maafisa sheria kuzungumzia mradi huo katika vituo vya radio pia
vipeperushi vinavyoelezea mradi wa Mapitio ya Mfumo wa Haki katika
Mashauri ya Madai vimesambazwa katika wilaya zilizopo kwenye mikoa hiyo.
Mikoa
inayotembelewa Maafisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni
Arusha, Mwanza, Dodoma, Iringa, Morogoro na Mtwara.
Wakiwa
katika mikoa hiyo Maafisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
wanaelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Tume katika kuboresha
mfumo mzima wa Utoaji Haki katika Mashauri ya Madai nchini Tanzania.
Mradi
wa Mapitio ya Sheria za Madai ni moja ya hatua zilizochukuliwa na
Serikali ya Tanzania chini ya Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara
Tanzania (BEST) ambao unalenga kuondoa vipingamizi vya kiuratibu na
kiutawala katika kufanya biashara.
Mapitio
hayo yanalenga kuboresha Mfumo wa Utoaji Haki za Madai Tanzania ili
kupunguza ucheleweshaji, gharama na ugumu wa utatuzi wa mashauri ya
madai ili kuendana na ibara ya 107 A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Katika mradi huo Sheria ya mwenrendo wa mashauri ya madai ni
mojawapo ya sheria zinazofanyiwa kazi.
Tume
kupitia mradi huo inafanya mapitio ya kanuni zinazohusu Mfumo wa Haki
za Madai tisa (9) zinazohusiana na uendeshaji wa mashauri ya madai.
Kanuni hizo ni pamoja na zinazohusu Tozo za Ada za Mahakama, Likizo za
Mahakama, Maafisa wa Serikali kuwakilisha Serikali Mahakamani, Tozo za
Ada kwenye Mahakama kuu, kanuni zinazohusui Lugha ya Mahakama na kanuni
za Maadili.
Kanuni
hizo zote ni changamoto zilizobainishwa na Tume baada ya kuzifanyia
mapitio katika Mfumo wa Haki za Madai na zimefanyiwa kazi ili kutoa
mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mfumo wa utatuzi wa migogoro ya
madai hapa nchini.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)