Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi wa
SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu Peter
Lupatu ambaye yupo Mkoani Rukwa kwa ajili ya ukaguzi wa bandari ya
Kasanga na vifaa vya usafiri wa majini katika ziwa Tanganyika ikiwemo
meli ya Mv Liemba na Mv Mwongozo. Mkuu huyo Mkoa alimuomba Mkurugenzi
huyo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya majini hususani Meli
ili kuepusha ajali mbaya zinaweza kujitokeza kama ilivyotokea kwa meli
za Mv Spice Islanders na Mv Skagit katika bahari ya Hindi. Alisema ajali
nyingi husababishwa na ubovu wa vyombo hivyo ambavyo vinahitaji
ukarabati wa mara kawa mara.
Mkoa
wa Rukwa unapakana kwa karibu sana na Nchi za Kidemeokrasia ya Kongo,
Burundi na Zambia ambapo mpaka wa nchi hizo upo katika ziwa Tanganyika.
Kwa kuona umuhimu wa kuziunganisha nchi hizo kibiashara Serikali imeamua
kujenga bandari ya Kasanga ambayo itakuwa kiunganishi kikubwa cha
kibiashara na nchi hizo. Sio bandari peke yake bali pia barabara za lami
kutoka Mkoa wa Mbeya (Tunduma)-Sumbawanga hadi Kasanga ilipo bandari
hiyo inaendelea kujengwa na inategemewa kukamilika mwakani 2013. (Picha
na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)