Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu Dk Vuai Lilaakitia saini
kwa niaba ya serikali ya mapinduzi zanzibar,Kulia ni Fundi Mkuu
Sathish Babu wa Kampuni ya M/S db Shapriya + Co.Ltd
---
Na: Nafisa Madai-Maelezo ZanzÃbar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana saini Ujenzi wa Barabara
mbili za Koani-Jumbi,Jendele ,Cheju hadi Kaebona na barabara ya
Kizimbani-Kiboje kwa kiwango cha lami ambao utagharimu shilingi bilioni
14.833.
Hayo yamefahamika wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya ujenzi huo
kati ya Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu na Kampuni ya M/S db
Shapriya + Co.Ltd yaliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini
Unguja.
Makubaliano hayo yametiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano na Miundombinu Dk Vuai Lila kwa niaba ya Serikali ambapo
kwa upande wa Kampuni hiyo iliwakilishwa na Fundi Mkuu Sathish Babu.
Akizungumza mara baada ya utiaji saini katika hafla hiyo Katibu Mkuu
wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Dk Vuai Lila, alisema fedha
hizo zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Kiarabu kwa Maendeleo ya nchi
za Afrika (BADEA), ambayo imetoa dola za marekani milioni 8 wakati
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa dola za kimarekani milioni
2.36.
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa BADEA itachangia shilingi bilioni
11.454 ikiwa ni sawa na asilimia 72.22, ambapo Serikali itachangia
shilingi bilioni 3.379 sawa na asilimia 22.78. Aidha amesema zaidi ya
shilingi milioni 900, atalipwa msimamizi wa mradi huo na BADEA, ambapo
Serikali italipa shilingi milioni 500 ikiwa ni fidia ya mazao na
nyumba katika maeneo yatakayopita barabara hizo.
Dk.Lila amesema mradi huo utaanza wakati wowote kuanzia sasa ambapo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 17.
Amesema ujenzi wa barabara hizo utaimarisha miundombinu ambayo ni
chachu ya maendeleo na kuwakwamua wananchi wa maeneo hayo kiuchumi
ili kuondokana na umasikini.
Amewataka viongozi na wananchi wanaaoishi karibu na sehemu
zitakazopita barabara kuzidisha ushirikiano ili kuleta ufanisi katika
ujenzi huo. "Mradi huu ni muhimu kwani utasaidia sana kusukuma
maendeleo ya nchi yetu hivyo tunaomba kuweko mashirikiano ili uweze
kukamilika kama ulivyokusudiwa", alisema Dk Lila.
Nae Mkandarasi Paul Bird, kutoka Kampuni ya DB Shapriya + Co.Ltd,
aliihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza ujenzi huo
kwa wakati sambamba na kujenga kwa kiwango kinachokubaliwa. "Naahidi
kuwa mradi huu utakwenda kama ulivyopangwa hivyo nataka mashirikiano
kwa wananchi na hata viongozi wa sehemu utakaopita mradi huo", amesema
Bird.
Kwa upande wake Diwani wa Koani Shaaban Jabu Kitwana, ameahidi kutoa
mashirikiano ya karibu ili kuona kuwa hakuna vikwazo vitakavyotokea
katika kipindi chote cha kazi hiyo.
Aidha Kitwana aliishukuru Serikali kusikia kilio chao cha siku nyingi
kwa kuwa itasaidia sana kuleta maenedeleo katika vijiji husika vya
mradi huo wa barabara.
IMETOLEWA NA
HABARI MAELEZO -ZANZIBAR.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)