MKUU WA MKOA WA RUKWA AKUBALI OMBI LA CHAMA CHA WAENDESHA BODABODA MKOA HUO KUWA MLEZI WA CHAMA CHAO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUU WA MKOA WA RUKWA AKUBALI OMBI LA CHAMA CHA WAENDESHA BODABODA MKOA HUO KUWA MLEZI WA CHAMA CHAO

Mwenyekiti wa Chama cha waendesha Bodaboda Mkoa wa Rukwa Ndugu Farjala Hussein akielezea mikakati ya kuimarisha chama chao pamoja na kuwasilisha ombi lao kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye hayupo pichani kuwa mlezi wa chama hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa chama cha waendesha pikipiki za biashara maarufu kama Bodaboda Mkoa wa Rukwa ofsini kwake alipotembelewa na vongozi hao kujadili mambo mbalimbali yanayohusu umoja wao ambapo walimuomba kiongozi huyo kuwa mlezi wa chama chao ambacho kinaanza kujijenga. Kulia ni Mwenyekiti mteule wa chama hicho ndugu Farjala Hussein. Mkuu huyo wa Mkoa alikubali ombi lao na kuwaahidi ushirikiano kwa kuwasaidia kuboresha huduma zao kwa wananchi wa Mkoa wake wa Rukwa.
Kikao hicho kilichumuisha pia maafisa ushirika kutoka Manispaa ya Sumbawanga ambao Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliwakabidhi majukumu mbalimbali ikiwemo daftari maalum la usajili wa madereva wote wa Bodaboda katika Mkoa wa huo kwa ajili ya utambuzi na utaratibu mwingine wa kiutendaji kwa ajili ya kuboresha huduma hiyo ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ajaili za mara kwa mara.Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages