MAAFISA WA JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAAFISA WA JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL

Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano (kushoto), akiipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). kwa utaratibu waliowawekea madereva wa malori yao ikiwemo vidhithiti mwendo na muda mfupi wa kuendesha magari hayo hivyo kupunguza ajali. Kahatano aliongoza ujumbe wa askari 9 kutembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam.
Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (katikati), akitoa maelezo jinsi mitambo ya kusafisha maji taka kuwa safi, wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni kiongozi wa ujumbe huo Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano. Kutoka kushoto ni, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi wa jeshi hilo, Theresia.
Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (katikati), akitoa maelezo jinsi mitambo ya kusafisha maji taka kuwa safi, wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni kiongozi wa ujumbe huo Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano. Kutoka kushoto ni, SSGT Enock Machunde, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi wa jeshi hilo, Theresia Kimaro.
Mtaalam wa Upishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (kulia) akitoa maelezo jinsi mitambo inavyochachusha bia wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages