Kumekuwa
na vurugu za hapa na pale, Polisi kupambana na vijana kwenye kituo cha
kupigia kura wakati wa uchaguzi mdogo kumchagua Mwakilishi wa jimbo la
Bububu Zanzibar jana jioni. (pichani) Polisi wa kuzuia ghasia
wakisaidiwa na kikosi cha Valantia kuwaondoa vijana waliojikusanya
karibu na kituo cha kupigia kura kwenye Shule ya Bububu.
Askari wakijiweka sawa kulinda amani eneo hilo.
Askari akimdhibiti mmoja wa vijana waliokuwa wakishinikiza vurugu eneo hilo.
Askari
akijaribu kuwaelekeza baadhi ya vijana utaratibu unaostahili katika
eneo hilo baada ya kumaliza kupiga kura ili kusubiri matokeo.
Baadhi ya vijana wakihamaki, baada ya kuona askari wakiwasili eneo hilo na kuanza kuwatawanya.
Askari
wakishushwa katika gari wakati wakiwasili katika eneo lililokuwa na
vurugu ili kudhibiti vurugu hiyo iliyokuwa imeandaliwa na baadhi ya
vijana, waliokiwa wakipinga matokeo.
| Kiongozi wa chama cha siasa (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari nje ya kituo cha kupigia kura. Picha zote na Martin Kabemba. |





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)