
Msimamizi
wa Kituo cha Afya cha Kendwa Nungwi Bwana Viola Franco kutoka Hoteli
ya Kimataifa ya Lagema Nungwi inayosimamia Kituo hicho akimkaribisha
Balozi SeifAli Iddi wakati alipofanya ziara ya kukitembelea Kituo hicho
kipya kuona hudumazinazotolewa

Muuguzi
Mkuu wa Hospitali ya Kivunge Dr. Ashura Shaib Mussa akimuelezea
majukumu yao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alipoitembelea Hospitalihiyo iliyopo Wilaya ya Kaskazini A.

Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Jamal Adam akimuelezea
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif changamoto wanazopambana
nazo Hospitalini hapo ikiwemo idadi kubwa ya wagonjwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akiwafariji
wazazi Hawa Mashauri na Fatma Mohd waliojifungua katika wodi ya Wazazi
ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alipofanya ziara ya awamu ya pili katika
taasisi za Wizara ya Afya Zanzibar.
--
Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar umeagizwa kuandaa Mpango Maalum kwa
ajili ya ujenzi wa Hospitali kubwa ndani ya Wilaya ya Kati
itakayosaidia kuipunguzia msongamano mkubwa wa Wagonjwa Hospitali Kuu
ya Mnazi Mmoja.
Agizo hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi alipokuwa akiendelea na awamu ya pili ya ziara yake ndani
yaTaasisi za Wizara ya Afya hapa Zanzibar.
Balozi Seif aliueleza Uongozi wa Wizara hiyo ya Afya kwamba Serikali
Kuu itakuwa tayari kuangalia uwezekano wa uwezeshaji wa ujenziwa
Hospitali hiyo muhimu kwa Jamii.
“ Tumefikia wakati kulingana na mahitaji ya huduma za Afya kwa wananchi
wetu kuwa na Hospitali kubwa katika kila Wilaya na hii kwa kiasi
kikubwa itaondosha vurumai isiyo ya lazima katika Hospitali yetu ya
Rufaa ya Mnazi Mmoja”. Alisisitiza Balozi Seif.
Balozi Seif alisema katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ameahidi kusaidia Vitanda 10 kwa ajili ya
wodi ya Wazazi na Serikali itajitahidi kutafuta mbinu za kutatuta
changamoto chengine zilizopo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliwapongezaWatendaji wa Hospitali hiyo kwa utendaji wao wa kazi licha
ya mazingira magumu wanayofanyia kazi.
Balozi Seif alishuhudia idadi kubwa ya Wagonjwa wanaopata huduma katika
Hospitali hiyo ambapo Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr.
Jamal Adam alieleza kwamba uwezo wa kuhudumia wagonjwa bado ni ule ule
tokea miaka ya thamanini wakati idadi ya wagonjwa imeongezeka mara
dufu.
Akiitembelea Hospitali ya Wazazi ya Muembe Ladu BaloziSeif alielezwa na
Watendaji wa Hospitali hiyo mfumo mpya ulioanzishwa wa makuz iya mtoto
kwa yule aliyezaliwa akiwa pungufu wa uzito ujuilikanayo kwa jina la
Kangaroo.
Mafunzo hayo tayari yameshaanza kufundishwa kwa Wazazi mbali mbali kwa
lengo la kujiweka tayari endapo Mzazi atatokezewa kujifungua Mtoto
mpungufu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikagua utendaji wa
wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge ambapo Muuguzi mkuu wa Hospitali
hiyo Dr.Ashura Shaib Mussa alishauri kuwepo kwa Kitengo cha Upasuaji ili
kuwapunguzia hatari wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya ghafla.
Dr. Ashura alisema ipo hatari na inaweza kusababisha kifo kwa mzazi
anayehitaji operesheni ya ghafla kwa kumsafirisha katika masafa marefu
kupatiwa hudumahiyo.
Akizungumza na Watendaji hao Balozi Seif aliwapongeza Madaktari,
Wauguzi pamoja na Wafanyakazi wote wa Hospitali ya Kivunge kwajuhudi
zao za kuiwekea mazingira safiHospitali hiyo.
Balozi Seif aliahidi kuipatia Hospitali hiyo Vitanda kumi na kuwataka
wajenge utamaduni wa kuvifanyia majaribio Vifaa vipya wanavyopelekewa
hata kama itakuwa bado kuvifanyia kazi pamoja na kuyapatia changa moto
matatizo yanayowakabili.
“Kama sijajua matatizo na changamoto zilizomo ndani ya Mawiza na
Taasisi za Serikali wakati mimi ndie Mtendaji Mkuu wa Serikali
nitashindwa kutoa maamuzi au ufafanuzi pale unapohitajika”. Alisema
Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimalizia ziara yake kwa kukaguwa
Hospitali mpya ya Wazazi iliyopo katika Kijiji cha Kendwa ambayo
imefadhiliwa na Uongozi wa Hoteli ya Kimataifa ya Lagema. Daktali Mkuu
wa Hospitali hiyo iitwayo R.G.F Matenity Clinic Dr. Hawa Kivembele
alimueleza Balozi Seif kwamba huduma za Hospitali hiyo ambazo ni bure
zilizoanza mapema mwezi huu zimelengwa kwa wanakijiji wa eneo hilo.
Hata hivyo Dr. Hawa alisema mbali ya wanakijiji haolakini pia Hospitali
hiyo hutoa huduma ya malipo kwa Wafanyakazi wa Hoteli zotezilizoko
katika ukanda huo
Na
Othman Khamis Ame,
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)