Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa
akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na
maandalizi ya mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka barani
Afrika Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.
---
Na.MO BLOG -Arusha
Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania Mh.
Theresia Huviza anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Rais wa Mazingira kwa
Afrika katika Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa mazingira unaofanyika Arusha
nchini Tanzania kuanzia kesho hadi tarehe 14 mwezi huu.
Waziri Huviza ataongoza kwa kipindi cha muda wa miaka miwili ambapo baada ya hapo nafasi hiyo itachukuliwa na nchini nyingine.
Mkutano
huo umefanikishwa na European Union, Ubalozi wa Norway, Global
Environmental Facility, UNEP na UNDP na wajibu mwingine ukifadhiliwa na
serikali yenyewe.Bajeti ya maandilizi ya mkutano huo imegharimu takriban
dola za kimarekani 350,000 sawa na shilingi za Tanzania zaidi ya
milioni mia 6.
Pichani
juu na chini ni Watoto wakifanya mazoezi ya wimbo maalum watakaoimba
kesho kwenye mkutano wa 14 wa mawaziri wa mazingira barani Afrika mbele
ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania
Mh. Theresia Huviza.
Harriet
Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(kushoto) akitoa
maelezo mmoja wa wadau wa mazingira aliyefika katika banda la Umoja wa
Mataifa lililopo katika jengo la AICC utakapofanyika mkutano wa 14 wa
mawaziri wa Mazingira.
Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu aktioa maelezo kwa
mmoja wa wadau ya namna Umoja wa Mataifa inavyoshirikiana na Serikali ya
Tanzania katika utunzaji wa Mazingira kupitia mpango wa mazingira
(UNEP) uliopo chini ya Umoja wa Mataifa.
Banda
la ROA OZONE ACTION PROGRAMME chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na UNEP
wakitoa maelezo katika kutunzaji wa mazingira kwa wananchi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)