BODI YA WAHANDISI KUADHIMISHA MIAKA 10 YA JUMUIYA YA WAHANDISI SEPTEMBA 6-7 MWAKA HUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BODI YA WAHANDISI KUADHIMISHA MIAKA 10 YA JUMUIYA YA WAHANDISI SEPTEMBA 6-7 MWAKA HUU

Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa wahandisi nchini  Mhandisi  Prof. Ninatubu  Lema (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya 10 ya  jumuia ya wahandisi  kuanzia tarehe 6-7 mwezi wa tisa mwaka huu. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Bodi hiyo iliweza kuwafutia usajili wahandisi 164 ambao walikiuka maadili ya kazi na kusimamisha miradi 12 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za uhandisi na taratibu za kiujenzi. Kulia ni Msajili wa Bodi Mhandisi Steven Mlote.
Msajili wa Bodi ya wahandisi nchini  Mhandisi Steven Mlote akijibu maswali ya waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Bodi hiyo iliweza kuwafutia usajili wahandisi 164 ambao walikiuka maadili ya kazi na kusimamisha miradi 12 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za uhandisi na taratibu za kiujenzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi  Prof. Ninatubu  Lema.
Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa wahandisi nchini  Mhandisi  Prof. Ninatubu  Lema (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu  sherehe za maadhimisho ya 10 ya  jumuia ya wahandisi  yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia tarehe 6-7 mwezi wa tisa mwaka huu. Kulia  ni Msajili wa Bodi Mhandisi Steven Mlote na Kushoto ni Msajili Msaidizi  Mhandisi Benedict Mukama.(Picha na Anna Nkinda – Maelezo)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages