MSHINDI wa shindano la Bongo Star Search (BSS) 2009 Pascal Cassian atazindua albamu yake ya nyimbo za injili iitwayo Yasamehe Bure kesho (Jumapili hii) katika Uwanja wa Fisi.
Albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo kama vile Chuki ya Nini, Nikumbuke na Mimi, Jina la Yesu, Mafuriko, Pesa, Baba na Usilie.
Albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo kama vile Chuki ya Nini, Nikumbuke na Mimi, Jina la Yesu, Mafuriko, Pesa, Baba na Usilie.
Akizungumzia albamu hiyo alisema
kuwa ina lenga kuwarudisha waliopotea kwa Mungu kwa kuwapatia ujumbe wa
neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.
Alisema kuwa akiwa kama kijana
ameamua kutumia muda, nguvu na akili zake nyingi katika kumwimbia na
kumsifia Mungu na hivyo ameamua kuwafikishia vijana, watoto na watu
wazima ujumbe kupitia nyimbo.
Pia akizungumzia sababu ya
kuzindulia albam yake katika eneo la uwanja wa Fisi alisema kuwa
kutokana na sifa mbaya ya eneo hilo ameamua ambapo limekuwa
likifahamika kama uwanja wa dhambi kutokana matukio mbalimbali ambayo
yanafanyika mahala hapo.
Alisema kuwa mgeni rasmi
anatarajia kuwa Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS)
Ritha Paulsen ambae ndie alieibua kipaji chake kupitia shindano hilo
mwaka 2009 wakati likiitwa BSS.
Uzinduzi huo pia utasindikizwa na
waimbaji wengine ambao ni Martha Mwaipaja, Sifa John, Joseph Kaka,
Beatrice na wengineo wengi.
Albamu hiyo ambayo ameirekodia katika studio mbalimbali imemchukua miezi mienne kuiandaa na itauzwa kwa shilingi 10000/=.
“ Mimi kwanza ninamshukuru Mungu
kwa kuniongoza mpaka kufikia hatua hii ya kuzindua albamu yangu na
ameweza kunifikisha hapa kupitia programu ya BSS ambapo ndipo
nilionekana uwezo wangu wa kuimba na kushinda na kumbe ilikuwa ndio
mwanzo wa safari yangu ya kumtumikia Mungu” alisema Cassian





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)